Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
NINAMFAHAMU Blandina Changula maarufu kama Johari, tokea akiwa underground wa maigizo katika kikundi cha Kaole, kabla hajapata jina linalomfanya kuwa mmoja wa wakongwe katika filamu Tanzania.

Wakati ule akichipukia, alikuwa mmoja kati ya chipukizi waliokuwa wanaonyesha wazi kwamba watakuja kuwa waigizaji wazuri. Anapatia sehemu nyingi katika sanaa, lakini utampenda zaidi Johari akiigiza sehemu inayohitaji majonzi, au mtu anayetaka kuhurumiwa.
Johari anaweza kutoa machozi wakati wowote akitaka. Anaweza kucheka kwa sauti na furaha dakika hii, lakini inayofuata akatoa machozi mengi hadi unashangaa. Napata wasiwasi ninapomuona akitoa machozi katika misiba, hujiuliza kama analia kweli kwa uchungu au ni mbwembwe tu za maigizo ili watu wajue ana uchungu!
Kama nilivyosema mwanzo, Johari ni mmoja kati ya waigizaji wasichana ninaowafahamu zaidi katika fani, pengine kuliko masistaduu wengi waliopata majina makubwa katika miaka ya hivi karibuni. Anajua kufanya kazi kwa kweli na ni lazima hawa waliomkuta, wampe heshima anayostahili kwa sababu anao mchango mkubwa sana katika game.
Ninafahamu kwamba Vicent Kigosi, wakati huo naye akianza kuogelea kwenye umaarufu wa filamu, alikuwa akitoka na dada huyu. Mara kadhaa nimewahi kuwakuta pamoja na kwa maana hiyo, hakuna mdau asiyetambua uhusiano wao.


Ni kutokana na uhusiano huo, ambao awali ulionekana kama wenye mwelekeo wa kuzaa ndoa, wawili hao walifungua kampuni yao, RJ, kila herufi ikiwakilisha mwanzo wa majina yao ya kisanii.
Lakini kama tunavyofahamu, wawili hawa walianza chokochoko katika uhusiano wao, baada ya kuwepo kwa taarifa za Ray kuchepuka na Chuchu Hans, binti mdogo aliyemkuta Johari katika fani. Mwanzo ilikuwa ni siri, lakini baadaye ikathibitika kuwa ni kweli kiasi kwamba hata Johari akakubali na kumwaga manyanga.
Sijui, labda kwa sababu ni wasichana, wawili hawa wamekuwa wakipigana vijembe kila wanapokaa pamoja au kukutana. Mara moja waliwahi kuripotiwa kupigana katika ofisi za RJ.
Wiki iliyopita, wawili hawa waliripotiwa kutukanana kwa mara nyingine na almanusura wazichape. Walikutana katika eneo ambalo Johari alikuwa ameweka kambi yake, Chuchu akiwa ameambatana na Ray.
Niseme wazi kuwa ingawa ni vigumu kuzungumzia hisia za watu kimapenzi, lakini kwa uzoefu wa wawili hawa, inaonekana kama wanaishi maisha flani yanayokwenda kinyume na ustaarabu wa kisasa.
Nianze na Chuchu. Mara zote ugomvi unapotokea, binti huyu huwa amemfuata Ray katika eneo analojua kabisa kuwa Johari atakuwepo, hivi kwa kutumia tu busara zake za kawaida, kwa nini huwa hajiepushi kusogelea? Kwa sababu anajua kuwa yeye alimpora mwenzake mtu wake.
Hivi anapokwenda ofisini kwa Ray kwa mfano, akijua kabisa Johari pia yupo, haoni kama anayakaribisha matatizo makusudi? Maana yake ni kuwa anakwenda pale akitamba kwamba hawezi kufanywa lolote!
Na Johari, kwa umri ulionao, huoni kama ni kujifedhehesha tu kumpigania mwanaume unayejua kabisa hana mapenzi nawe? Huhisi watu wanaweza kukuona ni mshamba wa mapenzi?
Binafsi, ninaamini kama ungekuwa huna habari nao, wao ndiyo wangejisikia vibaya na pengine wangekuwa wanajisikia aibu kuibuka sehemu ulipo kwa vile watasanifika.
Sasa wanapofikia sehemu wanapigana na kutukanana hadharani, sidhani kama kuna mshindi kati yao zaidi ya wastaarabu kuwaona kama watu wanaotafuta kiki, kama wenyewe wasanii wanavyosema.
Kwa majina na umaarufu walionao, walipaswa kuwa mfano. Kila siku watu wanadai wanawake ni dhaifu, lakini kwenye majukwaa wanakanusha sana ili hali katika uhalisia wanathibitisha. Kwetu sisi wanaume, tukishaamua kuachana na mwanamke, hatunaga bifu tena na mwanaume mwingine atakayekwenda kujitwisha mzigo!
Ushauri wangu kwa hawa wadogo zangu ni kujitambua, Johari kwamba enzi zake kwa Ray zilishamalizika na Chuchu kwamba kwa kuwa huyu ni wako, acha kumfuata mwenzio katika anga zake!
BONYEZA HAPA

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top