KAZI sana!
Mkazi wa Buguruni, Rukia Nassor amekimbilia Kituo cha Polisi Buguruni
jijini Dar kutoa taarifa ya bintiye Saida Said (18) (pichani)kutoroshwa
nyumbani kwake siku chache kabla ya ndoa.Alipofika kituoni hapo,
mwanamke huyo alimtaja mtu mmoja kwa jina moja la Shaban kwamba ndiye
aliyefanya kitendo hicho.
Akizungumza na Uwazi juzi, mmoja wa ndugu ambaye hakupenda jina lake
lichapishwe gazetini alisema mama huyo amekuwa akihaha kwa binti yake
kotoroshwa na mwanaume huyo tangu Septemba 25, mwaka huu ambapo kila
akimpigia simu hapatikana hewani.
Jeshi la polisi bado liko ndani ya msako
mkali ili kuhakikisha binti huyo anapatikana na hatua za kisheria
zinachukuliwa kwa mwanaume huyo.
“Mpaka sasa mama wa bi harusi hajatoa taarifa kwa bwana harusi wala
ndugu zake, amekuwa akimtafuta kimyakimya huku akimuomba Mungu binti
yake apatikane kwa vile mahari alishalipwa, sasa anaogopa ikifika siku
ya ndoa itakuwa aibu kubwa,” alisema ndugu huyo.
Ndugu huyo alisema Saida alitarajiwa kufanyiwa ‘kitchen part’ Oktoba
31, mwaka huu na kufuatia na ndoa Novemba 6 huku ikidaiwa kuwa, upande
wa bwana harusi michango inaendelea kama kawaida.
Jalada la uchunguzi kuhusu kutoroshwa kwa bi harusi huyo linasomeka Kumbukumbu; BUR/RB/10170/2014 KUTOROSHA.
Jalada la uchunguzi kuhusu kutoroshwa kwa bi harusi huyo linasomeka Kumbukumbu; BUR/RB/10170/2014 KUTOROSHA.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment