Mashine ya kutoa fedha ATM ya kwanza katika historia ya Somalia, imewekwa jijini Mogadishu. Baadhi ya watu hawakuelewa jinsi ya kuitumia, kwa sababu ni jambo geni mno, anaripoti mwandishi wa BBC Mohamed Moalimu, akiwa Mogadishu. Mashine hiyo iliyowekwa na benki ya Salaam Somali Bank, ipo katika hoteli moja ya kifahari, na inaruhusu watu kutoa dola za Kimarekani. Somalia ina mfumo usio kamili wa kibenki, na watu wengi hutegemea fedha zinazotumwa kutoka nje na ndugu na jamaa. Maendeleo ya Somalia yamepata kikwazo kutokana na zaidi ya miongo miwili ya mapigano.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment