Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
wema sepetu bongoclan.co.tz.
Baada ya migogoro mingi inayoikumba kundi la Bongo Movie na kusababisha baadhi ya wasanii wanaounda kundi hilo kulikimbia huku chanzo kikubwa kikidaiwa ni umbea, majungu na kutoaminiana kati ya wanakikundi. Jana kupitia akaunti yake ya Instagram Frola Mvungi ambae pia ni mke wa msanii H Baba ametangaza rasmi kujitoa katika Kundi hilo, huku sababu zikiwa ni kama za wenzake waliojitoa.
Hiki ndo alichokiandika katika post yake ya Instagram ” Dah..kutokana na mambo yanayoendelea bongo movie club ambayo Kiukweli hayaninufaishi chochote. Zaidi ya kuniongezea chuki kwa watu Bila sababu,Imekuwa ni tatizo kuwa upande wowote Bila malumbano,upendooo,fitna na roho mbaya zinazotengenezwa na sisi wasanii ndani ya club zilinifanya niondoke. Mara ya Kwanza but.! @stevenyerere2 alinishawishi Baada ya kuwa kiongozi nikiona mabadiliko nikarudi ila sasa.! stevenyerere ameng’atuka. Kwasababu ya kutetea wanyonge dah!waliobaki. Ndo wale walionifanya niondoke mwanzo..MAAMUZI magumu sina budi kusema kuwa ni bora nikae mwenyewe nifanye kazi zangu Bila problem Bila kufitinishwa na mtu yeyote..wale ni wasanii wenzangu nawapenda but sera za pale zimenishinda..natangaza. Kujitoa leo Rasmi siwezi migogoro ya Kila siku”

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top