Stori: Mwandishi Wetu
Ni shida! Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, chini ya Kamanda Mohammed Mpinga, limekuwa mstari wa mbele katika kusimamia maadili ya askari wake na kuwa mfano wa kuigwa lakini kuna baadhi wanalichafua, Ijumaa limenyetishiwa kamchezo kamili.
Polisi wa usalama barabarani wakidendeka.
HABARI KAMILI
Habari kamili ikufikie kwamba nyuma ya picha ya askari wawili, mwanamke na mwanaume wa usalama barabarani (matrafiki) wanaodaiwa kuacha kazi ya kuongoza magari na kwenda kufanya uchafu kichakani kuna utata mkubwa.
PICHA INASEMA
Picha hiyo inamuonesha trafiki mwanamke akiwa amepakatwa mapajani na trafiki mwanaume aliyekalia kitu kwa chini ili kupata balansi ya kumbeba mwenzake huku wawili hao ‘wakifanya yao’ wakiwa na sare za kazi.
TUJIUNGE NA VYANZO
Baada ya picha hiyo kusambaa kwa kasi ya moto wa kifuu kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii usiku wa kuamkia Jumatano wiki hii na kugeuka habari ya mjini, watu walikuwa na maoni tofauti huku baadhi wakipiga simu kwenye chumba chetu cha habari wakitaka kujua ukweli juu ya uwepo wa tukio hilo.
SIMU YA KWANZA
Simu ya kwanza iliyopigwa ilidai kwamba matrafiki hao ni maarufu katika Barabara ya Bagamoyo ambapo mara nyingi huongoza magari maeneo ya Tegeta jijini Dar.
Kamanda Mohammed Mpinga.
“Huyo mwanaume ni jamaa mmoja mpole sana anajulikana Tegeta na ana gari aina ya Baloon (Toyota).
“Huyo mwanamke, kwanza ni mke wa mtu lakini yupo bomba (mzuri) kinoma. Hata madereva daladala wanamjua maana amejaliwa, akitembea lazima atingishe,” kilidai chanzo hicho na kuongeza:
“Hapo ni maeneo ya Tegeta kwa sababu ukiangalia vizuri kwenye picha hiyo utaona nguzo ya umeme mkubwa wa Zanzibar.”
WHATSAPP
Wakati tukio likiwa ‘hot’, picha hiyo ilitumwa kwenye chumba chetu cha habari kwa WhatsApp huku ikiwa na maelezo kwamba tukio hilo lilijiri hivi karibuni mkoani Dodoma bila kufafanua maeneo gani kwa kuwa Dodoma ni kubwa.
NI KANDA YA ZIWA?
Chanzo kingine kilichozungumza na gazeti hili kilidai kwamba tukio hilo siyo la Dar wala Dodoma ni maeneo ya Kanda ya Ziwa.
“Hilo tukio ni la Kanda ya Ziwa. Itakuwa ni kwenye moja ya Mikoa ya Kanda ya Ziwa (kati ya Mwanza, Mara, Kagera, Shinyanga, Simiyu na Geita),” kilidai chanzo hicho.
IMETENGENEZWA?
Baadhi ya wadau wa jeshi hilo walidai kwamba kuna uwezekano picha hiyo ni ya kutengeneza (photo shop) kwa kuwa haikujulikana aliyeipiga na kwamba iliwezekanaje kuwapiga ili hali wakijua ni kinyume na maadili.
“Unajua kinachonifanya nihisi kama imetengenezwa ni namna walivyojiachia. Kwa vyovyote kuna kitu cha ziada kimefanyika kwenye hiyo picha,” alisema mmoja wa wachangiaji mtandaoni.
MTAALAM: HAIJATENGENEZWA
Ili kuondoa utata huo wa kutengenezwa au kutokutengenezwa, gazeti hili lilimwonesha picha hiyo, mtaalam wetu wa kompyuta (IT), Nicolaus Trac ambaye alithibitisha kuwa siyo ya kutengenezwa.
“Ni vigumu kuwa ni ya kutengenezwa kwa sababu kuu tatu.
“Moja, mandhari ni moja, ingekuwa ya kutengeneza kila mmoja angeonekana tofauti lakini mazingira yanaonesha imepigwa eneo moja.
“Pili, angalia mikono yao ilivyovaana au kuingiliana. Sidhani kama kuna mtaalam angeweza kuweka mikunjo hiyo ya mikono na vidole bila kukosea sehemu.
“Tatu, angalia huyo mwanamke alivyomkalia mwanaume, inaonesha kabisa kumkalia kwake kumesababisha mkunjo katika suruali kwenye paja la mguu wa kulia,” alifafanua Nicolaus.
PETE YAIBUA MAMBO
Mbali na kukemea tabia hiyo na ukosefu wa maadili hasa kwa mtumishi wa serikali, wapo baadhi ya watu mitandaoni walikuwa wakimshambulia trafiki mwanamke kwani picha ilimuonesha akiwa na pete ya ndoa kidoleni.
“Mimi sijui kama huyo trafiki ni mumewe lakini namuona ana pete ya ndoa maana yake kuna harufu ya mchepuko. “Lakini hata kama ni mumewe, kwa nini wafanye mambo ya chumbani hadharani tena na sare za kazi? Kama walikuwa wamezidiwa sana si wangeenda nyumbani?” Alihoji mwanamke mmoja aliyetumiwa picha hiyo kwenye WhatsApp.
KAMANDA MPINGA ANASEMAJE?
Gazeti hili lilimfowadia Kamanda Mpinga picha hiyo kwa njia ya WhatsApp ambapo alikiri kuwa nayo na kwamba wanaifanyia kazi kabla ya kuchukua hatua kali kwa wahusika.
Katika mahojiano ya Kamanda Mpinga na Global TV Online hivi karibuni, kamanda huyo alisisitiza kwamba kikosi chake kinaongoza kwa maadili na kwamba inapotokea tukio kama hilo hutolewa adhabu kali.
Credit GPL
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Next
MAPENZI: WEMA NA BABA, DIAMOND NA MAMA Kibonajoro.com ndio mtandao wako kwa habari za kitaifa/kimataifa, burudani, michezo, udaku na siasa, Tuwe pamoja huku pia >> Facebook
Previous
OOOOH MAMAAAA.! MWANAFA, LINAH WADENDEKA KWEUPEEE Kibonajoro.com ndio mtandao wako kwa habari za kitaifa/kimataifa, burudani, michezo, udaku na siasa, Tuwe pamoja huku pia >> Facebook
Je Umezisoma Hizi?
- VIDEO: Mama Wema Aeleza Beef yake na Man Fongo Kisa……..09 Sep 20160
NI Mama Wema Sepetu ambae ameingia kwenye headlines mitandaoni baada ya kutofautiana na mkali wa ...Read more ?
- Busu la Nelly Kamwelu shavuni kwa Diamond akiwa na Wizkid lawatoa povu mashabiki (Video)25 Aug 20160
Haipiti wiki bila Diamond kuwatoa povu mashabiki, hata kama alichokifanya si kwamba alidhamiria...Read more ?
- Picha za Masanja na Mke wake Zazua Maswali Kwa Mashabiki wake..Wadai Mke wa Mchungaji Apaswi Kuvaa Hivyo19 Aug 20160
Baada ya Harusi ya Mchekeshaji Masanja na Mkewe iliyofungwa Jumapili iliyopita wawili hao wameon...Read more ?
- AUDIO: Kitu Diamond kasema kuhusu yeye kuwa mapenzini na Hamisa Mobetto03 Aug 20160
Ukaribu wako kwenye mitandao ya kijamii siku za karibuni unaweza kuwa ulikukutanisha na stori...Read more ?
- Shamsa Ford Amuweka Wazi Mpenzi wake Mpya03 Aug 20160
Msanii wa filamu nchini Shamsa Ford amefunguka na kusema kuwa baada ya kuachana na mpenzi wake wa...Read more ?
- Madai: Flora Amwangukia Mbasha30 Jul 20160
Habari ya mjini ni Mwimba Injili Bongo, Flora Mbasha kudaiwa kumwangukia mumewe waliyetengana, Em...Read more ?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Post a Comment