Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Kijana Mmoja aliyefahamika kwa jina la Rajabu Issa (36), mkurya  mkazi wa Majengo mjini Shinyanga mkoani Shinyanga, hatimaye ametimiza lengo lake la kujinyonga baada ya kuwa akimwambia mke wake ipo siku atajiua.

Tukio hilo limetokea jana asubuhi huku chanzo cha kifo cha kijana kikiwa hakijulikani.

Mwili wa marehemu Issa ukiwa umebebwa kwa kupelekwa
 mochwari atika hospitali ya mkoa wa Shinyanga 

Akizungumza na mwandishi wetu ,mke wa marehemu bi Mgeni Hamis (23), alieleza kusikitishwa na kifo cha mme wake na kusema kuwa enzi za uhai wake alikuwa na tabia ya kumuambia mara kwa mara mkewe, kama utani kuwa ipo siku atajiua lakini kila akimuulizia sababu za kujiua nini ,alikuwa hamwambii na kumpa jibu kwamba hata akimwambia huwezi kumuelewa.
Mgeni alisema siku ya jana ambapo tukio hilo lilimetokea, ilipofika majira ya saa tatu asubuhi, Marehemu alimwambia mke wake kuwa aende kwao mtaa wa Ngokolo mjini hapa, akamsalimie mama yake mzazi (Mama yake na mwanamke),kutokana na mama huyo kuwa mgonjwa.

“Tumeamka vizuri na mme wangu, na ilipofika majira ya saa tatu asubuhi akaniambia niende nyumbani kwetu nika msalimiae mama yangu mzazi kwa vile ni mgonjwa, ndipo nikaondoka ,lakini baada  ya masaa machache, nikapigiwa simu na shemeji yangu wa Musoma kuwa mme wako mbona anatutumia meseji za vitisho, kuna nini huko?,”

“Ndipo nikaamua kumpigia simu mme wangu, ambapo iliita bila ya kupokelewa, nikachukua jukumu la kumpigia mpangaji mwenzangu ,Idaya Ibrahimu, akamwangalie mme wangu ndani mbona hapokei simu”


“ Alipoingia ndani kwangu ndipo akamkuta mme wangu kajinyonga juu ya dali, na amefariki dunia” alieleza mke wa marehemu.

Akielezea tukio hilo zaidi mpangaji mwenzake Idaya Ibrahimu, alisema baada ya kupigiwa simu hiyo majira ya saa tano asubuhi na mkwe wa marehemu, kwenda kumuangalia mme wake kama yumo ndani, ndipo alipomkuta kaning’inia juu ya dali akiwa na kamba shingoni na amesha poteza maisha.

Alisema baada ya kuona tukio hilo, ndipo alipochukua jukumu la kumtaarifa mke wa marehemu, majirani wenzake, pamoja na Jeshi la polisi, ambalo lilifika na kuuchukua mwili huo, na kuupeleka kwenye chumba cha kuhifadhia maiti kwenye hospitali ya mkoa wa Shinyanga.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga Justus Kamugisha amethibitsha kutokea kwa kifo cha kijana huyo, na kusema kuwa hakuna mtu yeyote anayeshikiliwa na Jeshi la polisi Juu ya kifo hicho, na uchunguzi bado unaendelea ilikubaini chanzo chake.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top