Mwandishi aliyechinjwa na IS Steven Sotloff
Wapiganaji wa dola ya Kiislam IS wamesambaza picha za video katika mitandao kwa lengo la kuonyesha kuchinjwa kwa mwandishi wa habari raia Marekani Steven Sotloff ambaye ni mmoja wa mateka wanaoshikiliwa na wapiganaji hao.
Mwandishi huyo Sotloff, mwenye umri wa miaka 31 ambaye alitekwa na wapiganaji hao mwezi August mwaka jana.
Wapiganaji hao wa katika picha hizo pia wameonekana wakimtishia kumuua mateka mwingine anayedhaniwa kuwa ni raia wa Uingereza.Mwezi uliopita Sotloff alionekana mwishoni katika picha za video zilizoonyeshwa kuhusiana na kuchinjwa kwa mwandishi mwingine wa Marekani James Foley.
Baada ya mauaji ya mwandishi wa awali Foley, mama mzazi wa mwandiashi wa Sotloff alitoa ombi maalumu kwa kiongozi wa wanajeshi hao Abu Bakr al-Baghdadi kutoa muua mtoto wake.
Marekani hivi karibuni ilifanya mashambulizi ya anga dhidi ya IS nchini Iraq.
Mwandishi wa masuala ya usalama wa BBC Frank Gardner amesema hatua hiyo ya wapiganaji wa IS ni kulipa kisasi kwa Marekani.
Baada ya kukamilisha hotuba yake muuaji huyo alianza kumchinja soltloff punde tu video hiyo ilizimwa.
Sekunde chache mateka mwingine raia wa Uingereza akaletwa DAvid Cawthorne Haines anaonekana kabla ya Ilani kutolewa kuwa hatma yake iko mikononi mwa taifa la Marekani.
Tazama video hapo chini (video inatisha onyo)Video hiyo imeanza na hotuba fupi ya Rais Obama. Baada ya hotuba hiyo, Mwandishi huyo anawekwa mbele ya kamera na kuuawa kikatili
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment