Ommy Dimpoz ambaye juzi alitimiza miaka kadhaa, alisherehekea siku yake ya kuzaliwa mbele ya mashabiki wa Fiesta wa mkoa wa Shinyanga.
Akizungumza na Bongo5 jana wakati akijiandaa kuelekea kwenye tamasha jingine la Fiesta lililofanyika Jumamosi hii mjini Geita, Ommy alisema kuwa ilikuwa surprise kubwa kwake kusherehekea siku yake ya kuzaliwa mbele ya maelfu ya mashabiki wa Fiesta.
“Jana (juzi) nilifanya one of the best shows kwa sababu pia nilikuwa na furaha ya siku ya kuzaliwa kwangu,” alisema. ‘Kwahiyo show ilikuwa nzuri na watu wamejionea hasa Shinyanga jinsi show ilivyokuwa kali.Ilikuwa ni siku kubwa sana katika maisha yangu kwa kusherehekea mbele ya maelfu ya watu.”
“Kile nilichokifanya kwenye show ni kikubwa sana licha ya hivi vingine vya kusema utakata keki na kula lakini kitendo cha kushare birthday na watu kama wale ni kitu kikubwa sana kwangu, vingine nitatoa sadaka kidogo ya kawaida,”alisema Ommy Dimpoz.
Katika hatua nyingine Ommy amewataka mashabiki wake kukaa mkao wa kula kwa video na audio mpya.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro








Post a Comment
Post a Comment