Home
»
Burudani
» LADY JAYDEE ADAI MAADU ZAKE WAMEBADILISHA WIMBO.....WALIANZA KUSEMA JAY DEE NI MGUMBA, WAKASEMA JIDE NI TASA.....SASA WAMEKUJA NA JIPYA TENA
Malkia wa muziki wa R&B, Lady Jay Dee amedai kuwa maadui zake wamebuni njia mpya ya kumwangusha, baada ya zile za awali kutofanikiwa.
Katika waraka mrefu aliouandika katika mtandao wa facebook, Lady Jay Dee alisema watu wasiopenda mafanikio yake wamekuwa wakitumia mbinu mbalimbali kumwangusha, lakini hata hivyo wameshindwa.
Jay Dee analalamikia habari iliyoandikwa juu yake kuwa amekuwa katika uhusiano mpya na kijana aliyemzidi umri, jambo analosema halina ukweli.
Jide ameandika: “Hata kama nimeachana na mume wangu, siyo sababu ya kunihusisha katika uhusiano na mwanamume mwingine yeyote. Habari hii imenivunjia heshima. Nafikiri lengo la uzushi huu ni kumfanya Lady Jaydee aonekane mtu asiyefaa.”
Habari hiyo ilipambwa na picha ambazo alizipiga mwenyewe kwa kutumia simu ya mume wake.
Aliongeza: “Ni vizuri kuzusha vitu ambavyo angalau unavijua, hizi picha zilipigwa kwa simu ya Gadner ambaye mnasema nimeachana naye, hamuoni kama mnawadanganya watu?”
Aliongeza kuwa huenda aliyeanzisha habari hizo ameona zile ambazo zilikuwa zikivuma wakati fulani, zimeshuka chati.
Alihoji: “Je, wimbo Jay Dee mgumba, Jay Dee tasa umeshuka chati ndiyo maana mmeamua kuleta mwingine?”
Hata hivyo, alisema lengo la wanaoanzisha uzushi juu yake ni kumdhoofisha lakini anaamini jinsi alivyoshinda vita ya kwanza, atashinda tena vita ya pili.
“Hata kama ndoa yangu haiko sawa, niacheni.Lakini isiwe sababu ya kuendelea kunichafua kwa maneno ya kizushi. Siyo lazima niandikwe, kwa sababu nilikuwapo kabla ya kuandikwa sana... nitaendelea kuwapo bila kuandikwa.”-Lady Jaydee
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Je Umezisoma Hizi?
- Alikiba Aelezea ‘King Kiba’ ilikotokea, Adai si Mtu wa Maringo09 Sep 20160
Alikiba ametoa ufafanuzi wa wapi #KingKiba ilitokea kiasi cha kuitumia katika sehemu nyingi.Akiong...Read more ?
- VIDEO: Mama Wema Aeleza Beef yake na Man Fongo Kisa……..09 Sep 20160
NI Mama Wema Sepetu ambae ameingia kwenye headlines mitandaoni baada ya kutofautiana na mkali wa ...Read more ?
- Mr Blue, Barakah Da’ Prince Wapatana08 Sep 20160
BAADA ya kutibuana kisa kikiwa Naj, hatimaye wakali wa Bongo Fleva, Mr Blue na Barakah Da’ Princ...Read more ?
- Ray C aonyesha muonekano wake mpya.........Mashabiki Wampa Ushauri Mzito08 Sep 20160
Msanii wa muziki Rehema Chalamila ‘Ray C’ ameonyesha picha yake ya kwanza toka asaidiwe na jeshi ...Read more ?
- Maneno ya Orijino Comedy kwa Jeshi la Polisi Kuhusiana na Kuvaa Sare za polisi23 Aug 20160
Hivi karibuni kundi la sanaa ya uigizaji la Orijino komedi liliingia matatani baada ya J...Read more ?
- Hamisa Mobetto Aukata Mzizi wa Fitina kuhusu Tetesi za Kutoka na Diamond23 Aug 20160
Kwa muda sasa mlimbwende wa Tanzania, Hamisa Mobetto amekuwa akituhumiwa kutaka kumpindua Zari th...Read more ?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Post a Comment