Talaka ya Amber Rose na Wiz Khalifa inaendelea kuchukua hatua mpya kila siku. Kwanza kuna ripoti kuwa alimsaliti Wiz na kisha yeye akasema ndiye aliyesalitiwa na mume wake na sasa inasemekana kuwa ataondoka na kitita kizito kutokana na ‘prenup’ ambayo wote walisaini.
Mama huyo wa mtoto mmoja alimtaka mume wake wasaini makubaliano hayo (prenuptial agreement) kabla hawajafunga ndoa mwaka mmoja uliopita ya kwamba atalipwa dola milioni moja wakiachana. Lakini kwa mujibu wa TMZ, makubaliano hayo yaliyo kwenye kurasa nane yanambana Amber ambaye anataka kulipwa fedha za zaidi ya ile dola milioni 1 iliyoandikwa ili kumsaidia kumlea mwanae
Taarifa hiyo imekuja baada ya Amber kutumia Twitter kukanusha kumsaliti Wiz.
Please stop with the fake stories. I would never ever ever cheat on my husband in a million years I think u guys know this…..
— Amber Rose (@DaRealAmberRose) September 25, 2014
Unfortunately my now ex husband can't say the same….
— Amber Rose (@DaRealAmberRose) September 25, 2014
I'm devastated and crushed but my main focus is Sebastian. Thank u for all the support in this difficult time.
— Amber Rose (@DaRealAmberRose) September 25, 2014
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment