*Asema malumbano ya viongozi hayawasaidii wananchi
WAZIRI
MKUU Mizengo Pinda ametoa saa 30 na kutaka kupatiwa majibu ni kwa nini
maelekezo aliyotoa kuhusu kiwanda cha kusindika nyama cha Mbeya
hayajafanyiwa kazi.
Ametoa
kauli hiyo leo mchana (Ijumaa, Agosti Mosi, 2014) wakati akizindua
Kongamano la siku tatu la Uwekezaji la Mikoa ya Iringa, Njombe na Mbeya
la mwaka 2014 ambalo limeanza leo kwenye ukumbi wa Benjamini Mkapa
jijini Mbeya.“Mbeya
inaweza kuwa na fursa kubwa ya viwanda vya usindikaji nyama, unga wa
mahindi ili kuongeza thamani ya mazao mnayozalisha katika mkoa wenu.
Nilipokuwa hapa ziara yangu ya mwisho 2012, niliagiza kiwanda hiki
kitafutiwe mwekezaji ili kianze uzalishaji. Jana nimeuliza kiwanda cha
nyama kimefikia wapi, naambiwa watu bado wanaongea. Wanaongea nini?,”
alihoji.“Mtu
akija kusikia habari ya kiwanda hiki atatuona ni wajinga tena ni
wajinga wa kujitakia, kisa watu bado wanazungumza… hiki kiwanda cha
nyama ni cha Mbeya na manuafaa yake ni kwa ajili ya wana Mbeya. Hivi
wahusika ni kwani hamuioni hiyo fursa?” alisema.
“Dk.
Mary Nagu watafute watu wa CHC waje hapa kujieleza ni kwa nini suala
hili limechukua muda mrefu. Kabla sijaondoka hapa Mbeya kesho nataka
nipate majibu kuhusu jambo hili,” aliagiza.
Katika
hotuba yake ya ufunguzi, Waziri Mkuu alisisitiza suala la watendaji wa
mikoa na wilaya kuchukulia kwa umakini suala la uwekezaji kwani
wasipofanya hivyo wao ndiyo watageuka kikwazo na kukwamisha maendeleo ya
wananchi wanaowaongoza.
“Ndugu
zangu wa Serikali za mitaa msiwe vikwazo, kuwezi wawezeshaji. Ninyi si
watawala bali ni waleta maendeleo kwa jamii. Natoa wito mshirikiane na
wafanyabiashara kuharakisha maendeleo ya wananchi mliokabidhiwa
kuwaongoza. Acheni kudai hongo, kwani badala ya kuwasadia jamii,
mtajikuta ninyi ndo mnakuwa vikwazo vya maendeleo,” alionya.
Alisema
Serikali za Mitaa zinapaswa kuwa wawezeshaji na siyo wakwamishaji wa
masuala ya maendeleo na ili kufanikisha hilo aliwataka wakuu wa mikoa
waanzishe one-stop centre katikangazi
ya mkoa na Halmashauri ili wawekezaji wanapofika katika mikoa yao
wasizungushwe na kukatishwa tamaa kwa sababu ya mlolongo wa taasisi
zilizopo.
“Uzoefu
unaonyesha kuwa baada ya kufanya makongamano kama haya, wawekezaji
wengi wanajitokeza lakini katika ngazi ya Mkoa na Halmashauri wanakosa
mahali ambapo wanaweza kushughulikiwa na kupata huduma bora kwa pamoja “One Stop Centre”. Hali hiyo huwafanya wakate tamaa.”
“Ninashauri kila Mkoa na kila Halmashauri iweke mfumo mzuri wa kuwapokea wawekezaji hususan kuwa na Mratibu (Focal Point) wa masuala ya uwekezaji ambaye ndiye atakuwa “One Stop Centre”
wa kushughulikia wawekezaji wanaojitokeza na kuwahudumia kwa ufanisi
bila urasimu. Ni imani yangu kuwa tukifanya hivyo, tutawezesha Kanda hii
kuwa kitovu kikubwa cha uwekezaji katika nchi yetu,” aliongeza.
Alisema
kila mmoja hana budi kuendelea amani na utulivu wa nchi ili uwekezaji
uweze kufanikiwa na kushamiri. “Hakuna uwekezaji endelevu na wenye tija
katikati ya fujo na migogoro, na uwekezaji utashamiri pale tu penye
amani na utulivu,” alisisitiza.
Mapema,
Waziri wa Nchi (OWM-Uwezeshaji na Uwekezaji), Dk. Mary Nagu alisema ili
uwekezaji uweze kuwanufaisha wananchi, ni lazima rasilmali za nchi
zigeuzwe kuwa bidhaa. “Ukiangalia chuma cha Liganga kipo pale miaka
mingi, bila kukigeuza kuwa bidhaa, bado hakiwezi kuwanufaisha wananchi
wetu,” alisema. Alisema bila uwekezaji hakuna uchumi, na bila uchumi
hakuna maendeleo na bila maendeleo hakuna maisha bora kwa kila
Mtanzania.
Katika
hatua nyingine, Wakuu wa mikoa ya Mbeya, Iringa na Njombe walipewa
nafasi ya kuzungumza na washiriki wa kongamano hilo ikiwa ni pamoja na
kuelezea fursa mahsusi zilizomo kwenye mikoa yao.
Mada
zitakazowasilisha katika kongamano hilo ambalo kaulimbiu yake ni
“Maendeleo ya Kiuchumi na Kijamii katika Nyanda za Juu Kusini” zinahusu
fursa za uwekezaji katika sekta za uchumi na miundombinu katika kanda
hiyo, fursa za uwekezaji katika sekta za huduma za jamii katika kanda
hiyo, fursa za uwekezaji katika kilimo cha mazao ya bustani (matunda,
mboga, maua na viungo) na mchango wa taasisi za fedha katika uwekezaji.
Nyingine ni mchango wa sekta binafsi katika uwekezaji, na nafasi ya MKURABITA katika kukuza mitaji ya uwekezaji.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
IJUMAA, AGOSTI MOSI, 2014
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WHATSAPP 0712-483 331
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu bonyza hapa
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro








Post a Comment
Post a Comment