Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This




 TFF Leo imetoa Ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom kwa Msimu mpya wa 2014/15 na Mechi za kwanza kuchezwa Jumamosi Septemba 20.
Ratiba hiyo, iliyosambazwa na Ofisa Habari na Mawasiliano wa TFF, Boniface Wambura, imezingatia michuano ya Chalenji itakayochezwa Novemba, Usajili wa Dirisha Dogo kati ya Novemba 15 na Desemba 15, ushiriki wa Klabu za Azam FC na Yanga kwenye Mashindano ya CAF ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho
Kwa mujibu wa Wambura, mechi zitachezwa Wikiendi tu ili kuongeza msisimko na kuwapa fursa Washabiki wengi zaidi kuhudhuria na katikati ya Wiki kuachwa wazi kwa ajili ya Mechi za Kombe la FA (Federation Cup).
Vilevile kutakuwa na Mechi kwenye Boxing Day na Siku ya Mwaka Mpya.
Ile Dabi inayongojewa kwa hamu Nchi nzima, Dabi ya Kariakoo, kati ya Yanga na Simba, itachezwa Oktoba 12 na Marudiano ni Februari 8.
Ligi itamalizika rasmi Tarehe 18 Aprili 2015.
RATIBA ya Mechi za Ufunguzi Septemba 20 ni kama ifuatavyo
Azam FC v Polisi Moro [Azam Complex, Dar es Salaam]
Mtibwa Sugar v Yanga [Jamhuri, Morogoro]
Stand United v Ndanda FC [Kambarage, Shinyanga]
Mgambo JKT v Kagera Sugar [Mkwakwani, Tanga]
Ruvu Shooting v Tanzania Prisons [Mabatini, Mlandizi]
Mbeya City v JKT Ruvu [Sokoine, Mbeya]
Septemba 21
Simba v Coastal Union [Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam]
Like ukurasa wetu wa facebook  ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu bonyeza hapa


Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top