Lady jaydee ameamua kujibu habari iliandikwa kwenye gazeti la udaku la Risasi kuwa na uhusiano na aliyekuwa mtuma salamu maarufu kwenye redio. Meddy Ahmed aka 'Mtoto wa vitoto'.

kwenye habari hiyo Risasi wanadai kuwa Jaydee ambaye anadaiwa kuachana na mume wake Gadner G Habash ameonekana mara kadha na Mtoto wa Vitoto na kwamba amewahi kuonekana akiwa na gari lake.
Kupitia Instagram, Jaydee ameandika:
Kuna habari za kuniudhi Ila imenichekesha kwahiyo mtoto wa Vitoto ndio bwana angu??? Basi sawa nashukuru naona mmenianza tena sasa picha za February Na nilizi post mwenyewe humu insta leo ndio mmeziona? Ukweli mnaujua mmeamua tu kuzingua .....wangapi wameshapiga picha na hiyo Range? Duuuh !!!!! Shkamoooni Moyo wangu chuma Pigeni mawe mpk mchoke Kama ambavyo mmekuwa mkifanya miaka yote na bado nipo hapa hapa."
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment