Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


MSHAMBULIAJI wa Yanga, Emmanuel Okwi, huenda akaiingiza hasara klabu hiyo na inaweza kulazimika kuvunja mkataba wake kama hatajiunga nayo mpaka usajili utakapofungwa Agosti 27 huku ikielezwa kuwa kuna ujanja ulifanyika wa kughushi barua ya timu iliyoelezwa kuwa ana mpango wa kujiunga nayo. Habari za uhakika kutoka ndani ya Yanga zinadai kuwa Okwi ni mchezaji anayewasumbua na amechukua fedha nyingi, lakini katika uchunguzi uliofanywa umebainisha kuna mmoja wa wanazi na kiongozi wa Yanga alishirikiana na kigogo wa Simba kutaka kumrubuni Okwi kwa kughushi barua kwamba kuna timu inamtaka. Habari zinasema kwamba viongozi wa Yanga walifuatilia kwa umakini juu ya madai ya kuwapo kwa timu inayomtaka na kubaini kuwa barua iliyotumwa Yanga haikutoka katika klabu hiyo ambayo hata hivyo haitajwi wazi. Yanga ilimsajili Okwi kwa Sh116milioni na inamlipa mshahara wa Sh6milioni kwa mwezi. “Tulibaini kuna ujanja ulifanyika kutoka kwa mmoja wa viongozi wa Yanga akishirikiana na mtu wa Simba kutengeneza uongo kwani klabu waliyosema inamtaka haina taarifa zozote, walitaka Okwi aachiwe ili ajiunge na Simba, hivyo bado tunaangalia jinsi ya kumchukulia hatua kiongozi huyo,” alidokeza kigogo wa Yanga. “Hapa kuna mawili, Yanga kuingia hasara kwa kuvunja mkataba na Okwi au Okwi kuendelea kuwepo katika timu, ila napo itategemea na kocha atakavyoamua kwani hataki mchezaji ambaye hana utayari wa kucheza, Okwi alisema atarudi ila hatujui ni lini.” Kwa upande wa Simba, ilielezwa kwamba suala la Okwi lilitinga katika vikao vya Kamati ya Usajili na kuleta mtafaruku mkubwa kwani wajumbe walio wengi hawakukubaliana na Okwi kurudi ingawa kigogo mmoja akawa anashinikiza na hakuungwa mkono.
Credit mwanaspoti
Bonyeza Hapa

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top