Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°
1- Kutoa zakatul-fitri,nayo ni wajibu kwa kila Muislamu, (mwanamume, mwanamke, mkubwa, mdogo, muungwana (huru) au mtumwa).*Watoto wadogo,Watumwa na pia Wanawake waliochini ya usimamizi wa Wanaume itawalazimikia zakah hio wasimamizi wao, ama Wanawake wanaojitegemea itawalazimikia wao wenyewe.

*Na inatakikana itolewe zakatul-fitri kabla ya Swalah ya iddi.
Imepokewa hadithi kutoka kwa Ibn ‘Umar (radhiya Allahu 'anhuma) amesema: Amefaradhisha Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa sallam) Zaka ya fitri (ya kumalizika Ramadhani) pishi ya tende au pishi ya shairi kwa mtumwa na huru (muungwana), mume na mke, mdogo na mkubwa katika waislamu, na akaamrisha (hiyo zakah ya fitri) itolewe kabla ya kutoka watu kuelekea katika Swalah (ya iddi). (Al Bukhariy na Muslim).
*Na wajibu ni kutoa pishi ya chakula maarufu katika mji uliopo (ambayo ni sawa na uzito wa kilo mbili na gramu mia nne (2.4 kg) takribani kwa nafaka kama mchele na mfano wake) (au thamani yake kwa baadhi ya wanachuoni).
2- Takbir, inasuniwa kuleta takbir baada ya kuandama (kuonekana) mwezi wa kumalizika Ramadhani, kuanzia kuchwa (kuzama) kwa jua mpaka wakati wa Swalah ya iddi. Na inasuniwa kunyanyua sauti kwa wanaume njiani, masokoni na hata majumbani.
3- Swalah ya iddi, kwa wanaume na wanawake.
*Na inasuniwa ifanyike katika viwanja, na hata akina mama walio katika siku zao (hedhi) inasuniwa na wao wahudhurie ingawa wao hawatoshiriki katika kuswali.
4- Na inasuniwa kula tende kwa idadi ya (witri) au chakula chengine hafifu kabla ya kutoka kwa ajili ya Swalah ya iddi al-fitri.
5- Pia inasuniwa kubadilisha njia wakati wa kwenda na kurudi kwenye Swalah ya iddi. Imepokewa hadithi kutoka kwa Jaabir (radhiya Allahu 'anhu) amesema: Alikuwa Mjumbe wa Allah (Swalla Allahu 'alayhi wa sallam) inapokuwa siku ya iddi akibadilisha njia (ya kwenda na ya kurudia). (Al Bukhary).
6- Kuvaa mavazi bora zaidi anayoyamiliki Muislamu.
*Na inatakikana kwa wale wenye familia kuwaandalia mavazi mazuri watu wa familia zao (bila ya kufanya israfu).

7- Na pia inasuniwa baada ya kumalizika Ramadhani kufunga siku sita katika mwezi wa mfunguo mosi (shawwali). Amesema Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa sallam): {Mwenye kufunga Ramadhani kisha akaifuatilizia siku sita katika mwezi wa shawwali (mfunguo mosi) inakuwa kama aliyefunga mwaka (mzima kamili).(Muslim).
8- Na tukumbuke ya kwamba siku hii ya iddi inakatazwa (ni haramu) kufunga ndani yake. Imepokewa hadithi kutoka kwa Abu Said Al khudriy (radhiya Allahu 'anhu) Hakika Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (Swalla Allahu 'alayhi wa sallam) amekataza kufunga katika siku mbili: Siku ya (iddi) alfitri na siku ya (iddi) ya kuchinja (iddi l-adh`ha)).(Al Bukhariy na Muslim).
TAQABBAL ALLAH MINNA WA MINKUM.
Chanzo Page ya Radio Imaan
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WHATSAPP 0712-483 331
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu bonyza hapa

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top