Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
 
Wanasayansi wanasema kunyamba au kujamba  ni afya
Kila mmoja wetu kwa wakati fulani huhisi kuvimbiwa na gesi nyingi tumboni.
Suluhu ya pekee hapa huwa ni kunyamba ili kupunguza gesi hiyo tumboni
Sasa Wanayansi katika chuo kikuu cha Exeter, nchini Uingereza, wanasema kuwa wamegundua harufu mbaya kama vile ya kushuta japo inachukiza kwa pua, ina manufaa makubwa kwa afya ya binadamu.
Wanasayansi hao wanasema kuwa harufu hiyo mbaya inaweza kuwa kinga dhidi ya magonjwa ya moyo na akili na hata Saratani.
Gesi au harufu mbaya ambayo hutokana na chakula kinachosagwa tumboni mwako inaweza kulinda baadhi ya viungo vya mwili wako.
Ndio! athari ni kile ambacho unakidhania: Eti watu wanauchukulia utafiti huu kumaanisha kuwa harufu mbaya inayotokana na mtu kunyamba inaweza kuzuia magonjwa fulani mwilini kama vile Saratani.
Utafiti huo uliochapishwa katika mtandao wa chuo kikuu cha Exter uligundua kuwa gesi hiyo inayojulikana kama Hydrogen Sulfide ambayo pia hupatikana katika Mayai yaliyooza, inaweza kuwa muhimu katika kutibu baahdi ya magonjwa.
"ingawa gesi ya hydrogen sulfide inajulikana kuwa na harufu mbaya na hupatikana katika Mayai yaliyooza pamoja na harufu ya mtu kunyamba, hutengezwa mwilini na inawezekana kuwa tiba kwa magonjwa fulani, ''asema Daktari Mark Wood,Profesa wa chuo hicho cha Exeter.
Gesi hiyo ina athari mbaya ikiwa katika viwango vikubwa , kwa mujibu wa utafiti huo. Watafiti wanasema licha ya harufu hiyo mbaya ya kunymba kuchukiza, ina uwezo mkubwa wa kupunguza uwezekenano wa mtu klupatwa na magonjwa kama vile, Saratani,Kiharusi, mshtuko wa Moyo na kuumwa na mifupa.
>>>>>BBC 



UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WHATSAPP 0712-483 331
 
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu bonyza hapa

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top