Liverpool wamemuulizia mshambuliaji wa
Southampton Jay Rodriguez, 24, baada ya uhamisho wa Loic Remy wa pauni
milioni 8.5 kuporomoka (Talksport), Manchester United wameambiwa
watatakiwa kulipa pauni milioni 79 kama wanamkata
kiungo wa Roma Kevin Strootmam, 24, licha ya mdachi huyo kuwa majeruhi
tangu mwezi Machi (Sun), beki wa Ubelgiji Jan Vertonghen, 27, amesema
atasaini mkataba mpya na Tottenham, licha ya Barcelona kumnyatia (Daily
Mirror), winga wa Real Madrid Angel Di Maria, anataka kujiunga na
Manchester United baada ya kughadhibishwa na PSG kumtaka kwa mkopo na
hataki kurejea Bernabeu (Daily Star), hata hivyo kocha wa Real Madrid
Carlo Ancelotti amesena anamtarajia kurejea kambini tarehe 5 Agosti
(AS), wakati huohuo gazeti la Marca linasema uhamisho wa Di Maria kwenda
PSG utatangazwa wiki ijayo katika mkataba wa pauni milioni 51. Juventus
watajaribu kutoa dau kumtaka mshambuliaji wa Chelsea Romelu Lukaku, 21,
kuimarisha kikosi chao ingawa wanakabiliana na ushindani mkali kutoka
Real Madrid (AS.com) Barcelona wameanza tena kumuulizia beki wa
Liverpool Daniel Agger, 29 (Le Figaro), Arsenal wamempa mkataba wa miaka
mitano kipa wa Real Madrid Iker Casillas, 33 (Bild) meneja wa Bayern
Munich Pep Guardiola anataka kumchukua kipa wa zamani wa Barcelona
Victor Valdes, 32 (AS.com), Barcelona wametangaza kumsajili winga kutoka
Brazil, Ferrao, 24 kutoka Tyumen ya Urusi (Mundo Deportivo). Tetesi
nyingine kesho tukijaaliwa. Tetesi hizi Na salim kikeke Kwa walioswali Eid leo- Eid Mubarak, kwa
wanoendelea kufunga, Saum Maqbul. Cheers!
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WHATSAPP 0712-483 331
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu bonyza hapa
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro








Post a Comment
Post a Comment