Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Filamu ya Scola ya mwigizaji Aunt Ezekiel imezuiwa kuingia sokoni na bodi ya Filamu Tanzania kutokana kuwa na “scene” zinasemekana kuwa kinyume na maadili ya Tanzania. Filamu hii imegundulika kuwa ina matatizo hayo baada ya muigizaji huyo kuipeleka kwenye bodi hiyo ili ikaguliwe kabla ya kuingia sokoni
Kupitia rafiki wa karibu na staa huyo ambaye alifafanua kuwa rafiki yake (Aunt) amekaliwa kooni na bodi hiyo lakini bado yupo katika mazungumzo kuona kama anaweza kuruhusiwa aendelee.

“Amejaribu kuwasihi ili kama kuna uwezekano iingie mtaani pasipo kuviondoa hivyo vipande kwani navyo vina umuhimu wake,” alisema rafiki huyo wa Aunt.
Alipotafutwa Aunt kuhusiana na suala hilo, alikiri kukaliwa kooni na bodi na kuomba apewe muda wa siku mbili ili aweze kulitolea ufafanuzi suala hilo lakini hakufanya hivyo, badala yake akasafiri nje ya nchi.
Mwaka jana mwishoni, bodi hiyo ya filamu ilimzuia mwigizaji Vincent Kigosi ‘Ray’ kuingiza sokoni sinema ya Sister Mary baada ya kuridhishwa na madai ya Kanisa Katoliki yalioainisha kuwa asilimia kubwa vipande vya sinema hiyo vilidhalilisha Ukatoliki.
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WHATSAPP 0712-483 331
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA
 

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top