Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
STORI: MAKONGORO OGING’

Kwa kweli duniani kuna mateso, lakini ya mtoto huyu yatima ni makali na maisha yake yapo hatarini kama hatawahi kupata matibabu. Fuatilia mkasa wake hapa chini ambao naamini utakuhuzunisha.
Kijana Twaha Sultan (16) ambaye ni yatima mkazi wa Kipawa Karakata, Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam akisimulia mkasa wake alikuwa na haya ya kusema:


Kijana Twaha Sultan akiwa na maumivu makali.

“Ndugu zangu, kufuatia maradhi ya ajabu yanayonisumbua sina raha ya maisha, niheri ningewafuata wazazi wangu waliotangulia mbele ya haki nikapumzike.“Nimekuwa mtu wa maumivu wakati wote, kulala na kula kwangu ni shida tupu mbaya zaidi ndugu ninaoishi nao hawana uwezo.

“Naamini kama wangekuwa na uwezo huenda ningekuwa nimepona maradhi haya yaliyoanza kama utani baada ya kunipeleka katika hospitali kubwa na kupatiwa tiba ya uhakika, kwa kweli nateseka jamani!
“Naumia zaidi ninapowaona vijana wa umri wangu wakiwa wanasoma na wenye furaha, wakati mimi nateswa na haya maradhi ambapo nisipopata tiba hatima yangu itakuwa kifo.

“Kabla ya kuanza kuugua, nilikuwa naishi na wazazi wangu huko Majengo, mkoani Tanga, bahati mbaya mwaka 2000 walitengana.
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WHATSAPP 0712-483 331

kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu bonyza hapa

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top