JAMBO limezua jambo! Yule jamaa aliyefahamika kwa jina la Huruma Bernard ambaye alidai kumfumania baba mwenye nyumba wake, Lugali akitaka kuvunja amri ya sita na mkewe, hatimaye ameamua kuhama nyumba.Fumanizi hilo liliripotiwa na gazeti hili, toleo la wiki iliyopita likiwa na kichwa cha habari, ‘VUNJA JUNGU GESTI’ ambapo Huruma alimfumania baba mwenye nyumba huyo kwenye gesti moja iliyopo Buguruni, Dar.
Bw. Huruma Bernard ambaye alidai kumfumania baba mwenye nyumba wake, Lugali akihama na mkewe kutoka nyumba waliyopanga.
Katika tukio la kuhama, Ijumaa iliyopita, wanahabari wetu walitonywa
na chanzo chao kuwa Huruma alikuwa anahama katika nyumba aliyokuwa
anaishi maeneo ya Ukonga, Dar baada ya kupewa notisi na baba mwenye
nyumba huyo ili kuondoa fedheha ya kumfumania gesti na mkewe.
...Mke na mume walifunga virago vyote tayari kwa kuhama.
Wanahabari wetu walipofika eneo hilo walimkuta Huruma na mkewe
wakibeba vitu ambapo jamaa huyo alisema kuwa amekubali kuondoka kwenye
nyumba hiyo baada ya kuona hakutakuwa na maelewano tena.
...Mke na mume wakiwa nje ya nyumba waliyopanga.
“Nimekubali kuhama kwani maelewano na baba mwenye nyumba hayakuwa mazuri tena baada ya kumfumania na mke wangu,” alisema Huruma.
...Mke na mume hao wakiondoka.
Alisema kwamba mkataba wake katika nyumba hiyo ulikuwa unatakiwa
umalizike Machi Mosi, mwakani lakini baada ya kumfumania wamekuwa na
bifu kubwa kiasi cha kukaribia kutwangana kila wanapopishana.
Shauri lao bado lipo kwenye Kituo cha Polisi cha Buguruni likiwa na
faili la kesi namba BUG/RB/6182/ 2014- UTEKAJI kwani baada ya fumanizi
jamaa huyo alidai alitekwa.
Credit..GPL
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WHATSAPP 0712-483 331
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment