Israeli
imeendelea kuivirumishia makombora Gaza kucha kutwa ,huku kikao cha
mawaziri wa baraza la Usalama kikitarajiwa huko Marekani kujadili
mapendekezo mapya ya wito wa kusitishwa mapigano kwa misingi ya
kibinadamu.
Afisa
wa ngazi ya juu wa umoja wa mataifa aliyeko Gaza Bob Turner, ameiambia
BBC kuwa wapalestina laki moja unusu , ambao ni asilimia 8 ya idadi ya
watu wa Gaza sasa wamekimbilia hifadhi kwenye shule za Umoja wa mataifa.
Idadi
ya raia wa Palestina waliouawa imezidi mia nane, huku mashambulio hayo
ya Israel ya angani majini na ardhini yakiingia siku ya kumi na nane.
Wanajeshi 32 na raia watatu wa Israel wameuawa katika muda huo.
Katika
ukingo wa magharibi, na Jerusalem mashariki raia wawili wa Palestina
wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa wakati waandamanaji waliokuwa na
hasira kuhusu mashambulio huko Gaza walipokabiliana na vikosi vya
Israel.
Katibu
mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki Moon anasema ameshtushwa na
kushambuliwa kwa shule ya Umoja huo iliyopo huko Beit Hanoun, ambako
mamia ya watu walifika kutafuta hifadhi.
Hata
hivyo Bwana Moon na waziri wa maswala ya kigeni wa Marekani John Kerry
wanaendeleza juhudi za kutafuta makubaliano ya kusitisha vita.
Kerry
alikuwa Cairo kukutana na waziri wa maswala ya kigeni wa Misri Sameh
Shoukry na Ban Ki-moon ambapo wanajaribu kuishinikiza Hamas kukubali
mwito wa kusitisha mapigano bila ya kuishinikiza Isareli kuondoa vikosi
vyake katika ukanda wa Gaza.
Israeli iliishambulia Gaza Julai tarehe 8 ikitafuta mbinu za kuzima mashambulizi ya makombora ya Hamas yanayotokea Gaza.
Mapema
leo maandamano makubwa yalifanyika katika ukingo wa Magharibi mwa
Palestina karibu na mpaka wake na Israel kupinga mashambulio
yanayofanywa na Israel.
Waandamanaji hao wakiwa na hasira walipambana na vikosi vya usalama vya Israel.
Hata hivyo mapambano makubwa dhidi ya vikosi vya usalama ilikuwa katika eneo la Qalandia katika mpaka wa Ramallah and Jerusalem.
>>BBC
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WHATSAPP 0712-483 331
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu bonyza hapa
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro










Post a Comment
Post a Comment