Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Gari la dude muda mfupi baada ya kukamatwa, Dude alitokea Polisi.
GARI la muigizaji maarufu wa filamu Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ limekamatwa na Polisi jijini Dar es Salaam likihusishwa na tukio la ujambazi linalodaiwa kutokea Kijitonyama Mpakani usiku wa saa 5.15 Julai 21 mwaka huu.Kwa mujibu wa chanzo chetu cha kuaminika, gari hilo aina ya Vitz lenye namba za usajiliT 360 BAJ, lilikutwa likiwa na vijana wawili ndani yake, waliotajwa kwa majina ya Seif Jafari na Longina Ramadhani, waliotaka kupora Bajaj yenye namba za usajili T 296 CSCiliyokuwa ikiendeshwa na Seleman Khalfani.
Inadawa kuwa muda mfupi baada ya kukamatwa, Dude alitokea Polisi na kulitambua gari lake, lakini maelezo yake hayakuwatosheleza Polisi hivyo kumshikilia katika kituo kidogo cha Polisi Mabatini hadi kesho yake alipodhaminiwa.
         Muonekano wa gari hilo kwa nyuma.
Waandishi wetu walifanya jitihada za kumtafuta Dude ili azungumzie taarifa hizo, lakini aliwataka kufuatilia jambo hilo katika kituo cha Polisi, akisema suala hilo lipo mikononi mwao.
Kulwa Kikumba ‘Dude’
Shauri linalomkabili msanii huyo limefunguliwa kwa Jalada namba .KJL/RB/6399/14 UNYANG’ANYI
Credit GPL
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WHATSAPP 0712-483 331

kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu bonyza hapa

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top