June 11, 2025 08:49:09 AM Menu
 

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Eto’o anaweza kuuhesabu 2014 kama mwaka mbaya kwake baada ya timu yake ya taifa kufanya vibaya kwenye michuano ya kombe la dunia lakini pia hana Club ya kuichezea baada ya kumaliza mkataba wake na Chelsea, kama hiyo haitoshi kwa sasa kilichombele yake ni kesi nzito Mahakamani. Kesi hizo za udhalilishaji ni kutokana na kusambaza picha za utupu, vitisho, ununuzi/uuzaji wa binadamu na udanganyifu zimefunguliwa kwenye Mahakama moja jijini Yaounde, Cameroon ambapo aliezifungua ni aliyekuwa mchumba wake wa zamani Hélène Nathalie Koah. Mapema wiki iliyopita Koah alifungua kesi hizo dhidi ya Eto’o ambaye amekana mashtaka hayo huku hili likiwa limetokea siku chache baada ya kusambaa kwa picha zake za utupu kwenye mtandao Facebook ambazo mhudumu huyo wa zamani wa ndege amesema zimesambazwa na Eto’o aliyekuwa mpenzi wake. Eto’o amekanusha kuhusika na hilo na katika kujibu mapigo mchezaji huyo anayeongoza kwa kutwaa tuzo nyingi za uchezaji bora barani Afrika, amefungua kesi ya matumizi mabaya ya fedha($410,755) alizompa Ms Koah kwa ajili ya kufungua taasisi ya kusaidia jamii wakati walipokuwa wapenzi.
Wakati hayo yakiendelea, kaa ukifahamu kwamba Mwanamke huyu alishawahi kuwaingiza kwenye ugomvi mwanamuziki Fally Ipupa na Eto’o baada ya kuwachanganya kimapenzi.
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WHATSAPP 0712-483 331

kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu bonyza hapa

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
29 Jul 2014

Post a Comment

 
Top