
Aliyekuwa mkufunzi wa timu ya soka ya Brazil Luiz Felipe Scolari
Brazil inatarajiwa kumtangaza
mkufunzi wake mpya katika mkutano na wanahabari siku ya jumanne kufuatia
kujiuzulu kwa kocha wa timu hiyo Luiz Felipe Scolari.
Scolari mwenye umri wa miaka 65 aliiongoza
Brazil katika semi fainali za kombe la dunia ambapo timu hiyo ilipata
kichapo kibaya cha mabao masaba kwa moja dhidi ya mabingwa wa kombe la
Dunia Ujerumani.Aliyekuwa kocha wa timu hiyo ambaye aliiongoza timu hiyo kati ya mwaka 2006 na 2011 huenda akarejea na kuchukua kazi hiyo.
Wengine wanaopgiwa debe kuchukua kazi hiyo ni mkufunzi wa kilabu ya Corinthians Tite,Mkufunzi wa kilabu ya Sau Paulo Muriciy Ramalho na Vanderlei Luxembourg ambaye aliwahi kuifunza timu hiyo kutoka mwaka 1998 hadi mwaka 2000.
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WHATSAPP 0712-483 331
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu bonyza hapa
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment