TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo iliishinda Zamalek ya
Misri kwa goli 1-0 kwenye mechi za makundi ya Ligi Kuu ya Mabingwa
Afrika siku ya Jumapili.
Mchezaji kutoka Zambia Rainford Kallaba alifunga goli pekee lililoipa
ushindi TP Mazembe. Kwa matokeo hayo ya Lubumbashi yanamaanisha kwamba
Mazembe wanaongoza kundi A kwa alama sita.
Wenzao wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, AS Vita Club wako nafasi ya pili, wakipitwa kwa alama mbili.
AS Vita walitoka sare ya 1-1 dhidi ya timu ya Sudan Al Hilal siku ya Ijumaa.
Kwa upande wa kundi B, Entente Setif ya Algeria walibanwa mbavu kwa sare 1-1 nyumbani kwao na Al Ahli Benghazi ya nchini Libya.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment