Gari aina ya RAV4 ikiwa chali baada ya
Kupata ajali mbaya Maeneo ya Kibaigwa ukiwa uanelekea Mkoani Dodoma.Mh:Mwigulu Nchemba akisaidia kuoka Majeruhi kwa Kuinua gari.
Gari aina ya RAV4 ikiwa imeshainuliwa tayari na Majeruhi wametoka walikuwa wawili.Kazi ya Kuondoa Betri ya Gari ndio inafanyika ilikuepusha Moto.Huyu ndiye alikuwa Dreva wa gari hii iliyopata ajali,amepata Michubuko kidogo.
Ajali
ndogo Imetokea maeneo ya Kibaigwa ikihusisha gari aina ya RAV4
iliyokuwa ikitokea Mkoani Morogoro kwenda Dodoma,Ajali hiyo mbayo
haijasababisha Kifo chochote imetokea majira ya Mchana wa Tar.08/06/2014
na Sababu ya ajali inatajwa kuwa ni Mwendo kasi wa Dreva na hatimaye
Gari Kumshinda na kupinduka.
Katika
tukio hilo Mh:Mwigulu Nchemba aliyekuwa akitoka Dodoma kuelekea
Morogoro kwenye Mkutano alilazimika Kusimama kwa Muda kwenye ajali hiyo
kwaajili ya Kutoka Huduma ya Kwanza kwa Majeruhi kama anavyoonekana
Pichani hapo Juu.Jambo hilo liliwafurahisha sana Wananchi waliokuwa eneo
la ajali na waliomba Viongozi wengine waige tabia hii ya Mwigulu
Nchemba ya Kushirikiana na Wananchi wakati wa Shida husuasani wanapoona
ajali barabarani,Ugonjwa,Misiba n.k wajitahidi kutoa Ushirikiano.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment