Msemaji
wa kundi la Pakistan Taliban Shahidullah Shahid amenukuliwa akisema kuwa
walitekeleza shambulizi hilo ilikumkumbusha rais wa Pakistan Nawaz
Sharif kuwa bado wepo nchini humu na kuwa kundi hilo litaendelea
kutafutia haki mamia ya watu wanaouawa bila ya hatia yeyote katika
mashambulizi ya ndege zisizo na ruban kwa misingi ya kuwasaka wapiganaji
wa wataliban.
Waziri
katika jimbo la Sindh , Qaim Ali Shah alisema kuwa wapiganaji hao
walikuwa wamejiandaa vilivyo kutokana na jinsi walivyotekeleza
mashambulizi hayo katika eneo la wageni mashuhuri katika uwanja huo mkuu
mjini karachi wa Jinna.
Inaaminika
kuwa 14 kati ya wale waliuawa ni maafisa wa usalama huku duru zingine
zikisema kuwa hata wahudumu wa ndege mbalimbali waliathiriwa katika
mkasa huo.
Mali ya thamani kubwa iliharibika lakini hakuna ndege iliyoharibiwa katika mashambulizi hayo.
Kuna hofu kuwa bado kuna mshambuliaji mmoja au hata wawili ndani ya uwanja huo.
Hata hivyo, Maafisa wanasisitiza kuwa sivyo.
Kwa sasa serikali imesema kuwa imedhibiti uwanja huo na kuwa sasa uko salama kwa usafiri wa ndege.
Ufyatulianaji
risasi na makabiliano baina ya wapiganaji wa kundi la Pakistan Taliban
na maafisa wa usalama wa Pakistan uliripotiwa kuanza upya muda mchache
uliopita katika uwanja mkubwa kabisa wa ndege wa Pakistan ulioko
Karachi.
Hii ni baada ya mashambulizi ya usiku kucha yaliyodaiwa kutekelezwa na kundi hilo la Taliban.
Takriban watu 19 waliuawa katika ufyatulianaji huo wa risasi, wengi wao wakiwa maafisa wa usalama wa uwanja wa ndege.
Maafisa wa usalama wa Pakistani wamesema kuwa washambulizi wote 10 waliuawa mwishowe na kuwa uvamizi huo ulikuwa umeisha.
Mwandishi wa BBC aliyeko Islamabad Shahzeb Jillani anasema uvamivi huo ulikuwa wa kijarisi na bila shaka wa kujitolea mhanga.
Huu ulikuwa uvamizi wa kijasiri katika uwanja mkubwa kabisa wa ndege nchini humo.
Baada ya
zaidi ya saa tano za mapigano makali na ufyatulianaji risasi , mkuu wa
usalama wa mji wa Karachi alisema kuwa wavamizi hao walikuwa
wameshindwa.
Lakini kidogo baadaye, milio ya risasi na milipuko ilisikika tena na kuzua taharuki.
Waokoaji walionekana wakirudi tena katika eneo la mashambulizi hayo.
Vituo vya habari vilionyesha picha za moto na moshi ukifuka tena kutoka kwenye paa ya uwanja huo.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment