
Rais Jose Mujica amesema maafisa wa FIFA wamuadhibu Suarez kwa unyonge wake
Rais wa Uruguay Jose Mujica
amewatukana maafisa wa FIFA kwa kuwaita ''kundi la watoto wa Mbwa'' au
"a bunch of old sons of bitches".
Hii ni baada ya maafisa wa shirikisho hilo kumpiga marufuku mchezaji wa nchi hiyo Luis Suarez.
Mchezaji huyo aliitaja adhabu hiyo ya marufuku ya miezi minne ikiwemo kutocheza mechi 19 za kimataifa kama adhabu ya kinazi.
Suarez alipata adhabu hiyo ambayo inasemekana
kuwa kali sana kuwahi kutolewa katika hoistoria ya kombe la dunia kwa
kumuua mchezaji wa Italia Giorgio Chiellini.
Rais Mujica anasifika kwa kutotafuna maneo yake pamoja na ukali wa matamshi yake.
Aliyatoa matamshi yake kupitia televishini ya
taifa alipokuwa anawapokea wachezaji wa timu hiyo baada ya kubanduliwa
nje ya michuano ya kombe la dunia katika awamu ya muondoano.
Rais huyo alifunika mdomo wake kwa mshutuko wa
kile alichosema , lakini wandishi wa habari tayari walikuwa
wamemrekodi.Pia aliwaambia kuyachapisha matamshi yake alipohojiwa ikiwa
alitaka kujirekebisha.
Rais huyo alisema kuwa FIFA ilimuadhibu Suarez kwa sababu ya maisha yake ya zamani ambayo yalikuwa ya unyonge.
Pia alitaja adhabu hiyo kama aibu kubwa sana kwa historia ya FIFA.
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment