Mama aliyetajwa kwa jina la Khadija Omari anayemtuhumu mzee huyo.
Kwa mujibu wa
Khadija ambaye ni mama mzazi wa mtoto anayedaiwa kuchukuliwa msukule
aitwaye Tausi, mwanaye huyo alifariki dunia Agosti, mwaka jana katika
mazingira ya kutatanisha.
Alisema kifo cha mwanaye kilimtatiza hivyo alikwenda kwa waganga wa
jadi ‘kuchungulia’ kama alifariki dunia kweli au ni mauzauza ndipo
akabaini kuwa kikongwe huyo ambaye alikuwa mwenye nyumba wake anahusika.
Mganga akijaribu kutoa dawa ya kurejesha mtoto.
Kufuatia
hali hiyo, Khadija aliamua kuondoka kwenye nyumba ya kikongwe huyo kwani
alikuwa akikutana na mauzauza kila kukicha na kutimkia mkoani Mwanza
huku akijipanga kutafuta mtaalam wa kumtoa mwanaye alipowekwa msukule.
Alisema hivi karibuni alirejea Dar na kutinga kwa kikongwe huyo akiwa na waganga wa jadi ili kumpata mwanaye.
Baadhi ya mashuhuda waliofika kushuhudia sekeseke hilo.
Hata
hivyo, zoezi hilo halikufanikiwa baada ya ndugu wa kikongwe huyo
kuingilia kati na kuanzisha timbwili la aina yake wakimtetea kwa madai
hawana imani kama anajihusisha na vitendo vya aina hiyo.
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA
Post a Comment
Post a Comment