MTOTO
aliyefahamika kwa jina la Najma Benjamin (7) amefariki dunia papo hapo
baada ya kugongwa na gari maeneo ya Bayuni Sheratoni, Kata ya Chanika,
Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam.Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Ilala, Ally Omary Mnzava, amesema kuwa huko Barabara ya Chanika,
gari aina ya Toyota Noah yenye namba T 611 CUN ikiendeshwa na Kasimu
Ally (22) mkazi wa Chanika Mwisho, imemgonga mtembea kwa miguu ambaye ni
mtoto huyo.
Mnzava
amesema mtoto huyo amefariki dunia papo hapo baada ya kugongwa na gari,
ambapo dereva kwa sasa amekamatwa na maiti kuhifadhiwa katika Hosptali
ya Taifa Muhimbili huku upelelezi ukiendelea.
Post a Comment
Post a Comment