
Watu
watatu wamekufa na wengine kumi wamejeruhiwa baada ya gari walilokuwa
wakisafiria aina ya Noha kupasuka tairi ya nyuma na kubingirita mara
tatu katika kijiji cha Januka manispaa ya Singida.
Akithibitisha
kitokea kwa vifoo hivyo mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Singida
daktari Deogratias Banuba amesema wamepokea maiti mbili wakiwa wamesha
fariki eneo la tukio akiwemo dereva wa Noha bwana Enock Mbaga, binti
Ajira Juma na maiti nyingine ya Bi Tatu Bunku ambaye alikuwa herd
mistres Ngimu sekondari amefia katika hospitali ya mkoa wa Singida .
Daktari
Banubasi amesema majeruhi kumi wamepatiwa huduma ya kushonwa sehemu
mbalimbali za miili yao na wanaendelea na matibabu ,pia hakuna majeruhi
ambaye atapatiwa rufaa .
Mmoja
wa majeruhi akiongea kwa shida huku akiwa amelazwa katika hospitali ya
mkoa wa Singida bwana Ramadhani Mlenga amesema gari halikuwa katika
mwendo wa kasi na gafla likaacha njia na kupinduka mara tatu.
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment