Siku chache baada ya kuachiwa kwa dhamana katika kesi ya kudaiwa kumbaka
shemejiye, mwimbaji wa Injili na mfanyabiashara Bongo, Emmanuel Mbasha
amedaiwa kuibiwa hati za nyumba na viwanja.
Chanzo makini kilichomo ndani ya familia, kimedai kuwa mara baada ya
Mbasha kujitokeza na kuwekwa mahabusu Juni 17, mwaka huu, mtu
asiyejulikana alikwenda nyumbani kwa mfanyabiashara huyo,
Tabata-Kimanga, Dar na kukwapua hati za nyumba na viwanja mbalimbali
anavyovimiliki.
“Mbasha hakukuta kitu pale nyumbani, vilikombwa vyote sijui na nani.
Inauma sana kwani mtu ndiyo kwanza ametoka mahabusu halafu anakuta
nyumbani kwake hakuna vitu muhimu kama hivyo, inasikitisha sana,”
kilisema chanzo hicho.
Kikizidi kumwaga data, chanzo hicho kilisema katika vitu vilivyoibwa
ni pamoja na nyaraka mbalimbali zikiwemo hati za viwanja kadhaa
vilivyopo Iringa, kadi ya gari na vitu vingine vidogovidogo.
Baada ya kunyaka madai hayo, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Mbasha ili kujua ukweli wa ishu hiyo ambapo alipopatikana alikiri kutovikuta vitu hivyo muhimu nyumbani kwake.
“Ni kweli kama ulivyosikia ila nisingependa kuzungumzia kila kitu kwa sasa nahitaji kupumzisha akili,” alisema Mbasha.
Mbasha aliyetoka kwa dhamana Juni 19, katika kesi hiyo ya kudaiwa
kubaka iliyosomwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, kesi yake itatajwa
tena Julai 17, mwaka huu.
Chanzo:Ijumaa wikienda
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment