MTOTO
mwenye umri wa miaka 14, mkazi wa maeneo ya Mghalani, mkoaniMtwara,
ambaye ni mfanyakazi wa ndani ‘Hausigeli’, anadaiwa kubakwa na
mwajiri wake na kumsababishia maumivu makali.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Maisha Maganga, alisema jana
kuwa tukio hilo lilitokea Juni 16 na kwamba baada ya kufanya ukatili
huo, mwajiri huyo aliyefahamika kwa jina moja la Sharifu, alitokomea
kusikojulikana.
Kamanda Maganga alisema ili kufanikisha azma hiyo, mtuhumiwa huyo
alitumia fedha kumlaghai mtoto huyo kisha kumbaka na juhudi za
kumtafuta zinaendelea.
Alisema Jeshi la Polisi linalaani vitendo hivyo viovu vikiwemo vya
ubakaji na hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa watu wote
watakaojihusisha na vitendo hivyo.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment