Kocha mpya wa klabu ya Yanga Marcio Maximo.
Aliyekuwa
kocha wa Timu ya Taifa ya hapa nchini Maxio Maximo kutoka Brazil
amepata fursa ya kurudi tena hapa nchini, kuja kuisuka vyema timu ya
Yanga ili iweze kucheza katika michuano ya kimataifa.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari kwenye makao makuu ya klabu ya Yanga, Jangwani,
wakala aliyemleta Maximo, Ally Mlee alisema kuwa, ilimchukua miaka 3
kumuomba kuja hapa nchini kusuka timu ya yanga, kwa kujali kwake na
ukarimu wa watanzania amekuja tena hapa nchini na amesaini mkataba wa
miaka miwili.
Kwa
upande wake Maximo alisema kuwa, amefurahi kuja kusuka timu ya yanga na
anamatumaini itafanya vyema katika michuano mikubwa nje ya nchi lakini
hata katika ligi ya hapa nyumbani.
“Watanzania
ni wakarimu sana ndio maana nimekubali kuja tena hapa nchini kuinoa
Yanga, lakini pia ujio wangu nimekuja na kocha msaidizi ambaye
atanisaidia kusimamia na pia nitapendekeza wachezaji wazuri kutoka
katika timu kubwa huko Ulaya, ili waje kuchezea Yanga lakini pia ni
fursa kwa wachezaji wa yanga kujinoa kupitia wachezaji wakubwa,” alisema
Maximo.
Siku ya Jumatatu timu ya Yanga itaanza mazoezi na mwalimu huyo mpya, maandalizi ya kujiandaa na ligi mbalimbali.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro








Post a Comment
Post a Comment