MFANYAKAZI
wa Kampuni ya simu ya Tigo, (MIC T Ltd.), jijini Arusha, Mwita Makore,
amekutwa amekufa nyumbani kwake maeneo ya Kimandolu huku akiwa na kamba
za viatu shingoni kuashiria kwamba alijinyonga nazo kwa kujitundika
kwenye bomba la bafuni kwake.
Hali
hiyo imezua gumzo miongoni mwa wakazi wa jiji la Arusha wakihoji
inawezekanaje mtu kujinyonga kwa kamba ya viatu hadi kufa huku wengine
wakihoji uwezekano wa mwili wa mtu mzima kuning’inia kwenye bomba la
bafuni.
Habari
kutoka eneo la tukio zinadai kuwa mwili wa Makore ambaye alikuwa
kitengo cha ‘store’, ulibainika Juni 20, mwaka huu baada ya kutoonekana
wala kupatikana kwa simu zake za kiganjani kwa siku mbili mfululizo,
hali iliyowalazimu wafanyakazi wenzake kwenda kumtafuta nyumbani kwake
na kubaini kifo chake.
Mmoja
wa wafanyakazi wa kampuni hiyo jijini humo aliyezungumza kwa sharti la
kutotajwa jina lake, alisema mara ya mwisho Makore kuingia ofisini
ilikuwa ni Juni 18, mwaka huu.
“Unajua
yeye kazi yake haimlazimu kuwa ofisini muda wote, hivyo akishamalizana
na wateja wake huondoka, hivyo siku ya Alhamisi hakuja kabisa ofisini,
lakini hakuna aliyekuwa na wazo kama kakutwa na jambo baya.
“Alikuja
mteja anayehitaji vocha, ikabidi apigiwe simu, simu ikawa inaita
haipokelewi, siku inayofuata wakaja wateja wengine, Mwita akapigiwa simu
zake zikawa zinaita tu lakini hazipokelewi.
“Yule
mteja akachukia akaamua kupiga simu makao makuu kueleza usumbufu
anaoupata, ndipo nao wakawapigia viongozi hapa wakawaeleza kama hapokei
simu kwanini wasimfuatilie nyumbani kwake pengine amepata matatizo,”
alisema mfanyakazi huyo.
Alisema
kuwa walipofika nyumbani kwake walikuta gari ya Kampuni ya Tigo ikiwa
imeegeshwa vizuri, lakini funguo zake ziko ndani na milango imerejeshewa
tu huku kwenye mlango wa kuingia ndani kwa Makore kukiwa na viatu vyake
na walipopiga simu zake, wakasikia zikiita kutoka ndani ndipo wakaamua
kuingia ndani.
“Tulipoingia
pale mezani tulikuta kuna chupa ya soda, na simu zake tatu pamoja na
kadi zake za benki, tukaendelea kuangalia maeneo mbalimbali ya nyumba
hiyo ndipo tukamkuta Makore bafuni na kamba ya viatu shingoni,” alisema
mfanyakazi huyo wa Tigo.
Mwananchi
mwingine anayeishi maeneo ya Kimandolu, alisema tukio hilo
limewashangaza sana kwani Makore alikuwa kijana mtaratibu asiye na makuu
na alikuwa mpenzi wa mchezo wa pool table.
Kamanda
wa Polisi mkoani Arusha, Liberatus Sabas, alithibitisha kutokea kwa
kifo hicho alichodai ni cha kawaida kwani amekutwa amekufa nyumbani
kwake na hakuna mahali palipovunjwa.
“Achana
na habari za barabarani, amekutwa amekufa nyumbani kwake, hakuna mahali
pamevunjwa, hiyo ni ‘natural death’,” alisema Sabas
via>>>Tanzania daima
kama huja like ukurasa wetu wa facebook kwa habari zaidi BONYEZA HAPA
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment