SAKATA
linalohusu kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited
(IPTL), limechukua sura mpya baada ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati
na Madini, Eliakim Maswi, kuwashambulia kwa maneno makali, wabunge
wawili Zitto Kabwe wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA) na David Kafulila wa
Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi).
FikraPevu ilikuwapo
wakati Maswi akitumia maneno makali kwa kuyarudia, akikejeli nyaraka
zinazotajwa kuwa ni ushahidi wa jinsi IPTL ilivyouza hisa zake na fedha
kutolewa kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT) katika akaunti maalumu ya
pamoja (Escrow), akisema nyaraka hizo ni karatasi za kufungia vitumbua
zinazosambazwa na wabunge hao aliowaita “washenzi”.
Kauli
hiyo ya Maswi imekuja siku mbili tu baada ya Mwanasheria Mkuu wa
Serikali (AG), Jaji Frederick Werema kushambuliana na Kafulila kwa
maneno makali malumbano yao yakianzia ndani ya Bunge na kuendelea
walipotoka, kila mmoja akiamini kauli aliyoitoa ilikuwa ni sahihi.
Werema
alimfananisha Kafulila na tumbili na yeye kumuita mwanasheria huyo
mwizi. Tumbili ni mnyama wa porini wakati mwizi ni mtu anayetenda
uhalifu kwa kuchukua kitu au mali isiyo yako.
TAZAMA VIDEO HAPA CHINI au BONYEZA HAPA
kama huja like ukurasa wetu wa facebook kwa habari zaidi BONYEZA HAPA
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment