HUKU
watu karibia 60 nchini kenya wakiuawa kwenye mashambulizi ya kigaidi,
katika hali isiyo ya kawaida nchini Tanzania, walinzi wa Maduka ya
Mlimani City jijini Dar wamejikuta wakipata mchecheto wa aina yake baada
ya kitu kilichodhaniwa ni bomu kukutwa kwenye eneo la kuegeshea magari.
Tukio
hilo lilitokea Juni 16, mwaka huu ambapo kwa mujibu wa shuhuda
aliyeomba kusitiriwa jina, aliona gari dogo jeupe likiangusha kifaa
hicho kilichodhaniwa ni bomu kisha likatoweka.
Chanzo hicho kilizidi kudai kuwa
baada ya gari kutoweka, dada mmoja alipita eneo hilo na kukuta kitu
hicho kilichofungwa nyaya kikiwa ndani ya mfuko, akashtuka na kwenda
kumtonya mlinzi wa eneo hilo ambaye alifika mara moja na kuwaita
wenzake.
Taarifa
za uwepo wa kifaa hicho ziliwafikia waandishi wetu waliokuwa wakipiga
doria katika eneo hilo na haraka wakasogea karibu kuwashuhudia walinzi
hao wa Kampuni ya Ulinzi ya Omega wakiwa wamekizunguka kifaa hicho kwa
umakini mkubwa.
Walinzi
hao walimuita kiongozi wao ambaye alifika na kukichunguza kifaa hicho
ambapo alipokifungua aligundua ni betri bovu la pikipiki.Waliichukua
betri hiyo na kuitupa huku wakitawanyika kurudi kwenye maeneo yao ya
ulinzi.
Eneo la Mlimani City.
Maoni ya Mhariri
Kutokana na kuwepo kwa matukio ya
kigaidi yaliyotokea nchini Kenya hivi karibuni, ni vyema jeshi la
polisi likawa na tahadhari katika maeneo yanayokusanya watu wengi kama
Mlimani City.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment