Kufuatia
kifo cha mtoto Nasra, almaarufu kama ‘mtoto wa boksi’, kuna kila dalili
kwamba kifo chake kimetokana na maradhi aliyoyapata wakati akiwa
anaishi kwenye boksi. Kwa
kuwa imethibitika kwamba mtoto alifariki kutokana na ugonjwa wa
pumu—kufuatia kufungiwa kwenye mazingira machafu, kutoogeshwa na kupigwa
na baridi masaa 24, na kwa kuwa wahusika waliokuwa wakimfanyia ukatili
huo tayari walishakamatwa na kufunguliwa mashitaka ya kula njama za
kumtesa mtoto huyo mdogo asiyekuwa na hatia na asiyeweza kujitetea,
mawakili wanaosimamia kesi hii watabadilisha masitaka ya kesi na kuwa
KESI YA MAUAJI YA KUKUSUDIA.
Adhabu
kwa mtu anayeua kwa kukusudia ni KUNYONGWA MPAKA KUFA. Kwa hiyo,
wahusika wanasubiri kunyongwa hadi kufa pindi hukumu ya kesi hii
itakapotoka. Na kwa kuwa kuna ushahidi wa kutosha
kuwatia hatiani hawa wanadamu wasokuwa na haya, wajiandae kupokea
kitanzi ili liwe fundisho kwa washenzy wengine wenye tabia za kinyama
kawa hawa wendawazimu.
NIONAVYO:
Natoa
wito kwa watanzania wenzangu kutoa taarifa polisi haraka pindi waonapo
ukatili wowote dhidi ya wanyonge, hasa watoto wadogo, ili sheria ichukue
mkondo wake. Tatizo la watanzania walio wengi ni kwamba hatujaliani.
Unaweza ukamuona mzazi/mlezi akimtesa mtoto lakini ukakaa kimya. Kufanya
hivyo ni kutomtendea haki yule kiumbe anayeonewa au kunyanayaswa.
Tuweni na huruma kwa viumbe hawa wa mwenyezi Mungu wanaoonewa bila
sababu za msingi huku wakiwa hawawezi kujitetea kwa namna yoyote ile.
Tukio la mtoto Nasra, ambaye Mungu amemuita kwake, liwe fundisho kwa
watu wengine wanaofumbia macho ukatili kwa watoto na wanyonge.
Nawasilisha.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment