Inaweza kuonekana ni kituko cha aina yake, lakini ni kweli
kimetokea kwenye Ukumbi wa Bunge la Kaunti ya Nairobi na kuwaacha
wabunge vinywa wazi.
Katika hali isiyo ya kawaida, boksi la kondomu
lilikutwa ndani ya ukumbi huo na kuwashtua wabunge wote akiwamo spika wa
bunge hilo.
Mwakilishi wa eneo la Karura, Kamau Thuo ndiye
aliyekuwa wa kwanza kuliona boksi hilo na kuwashtua wabunge wengine hali
iliyoibua mjadala mzito.
Kutokana na sintofahamu hiyo Spika Alex Ole Magelo
aliwataka wahudumu kufungua boksi hilo kujua kilichomo ndani yake ndipo
walipokuta kondomu.
“Nafahamu wote humu ni watu wazima, lakini
ninachoshangaa ni nani ambaye ameleta kondomu hizi ndani ya ukumbi huu,”
alihoji Spika Magelo.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Afya, Manoah
Mboku aliwaondoa hofu wabunge na kueleza kuwa kondomu hizo zilipaswa
kuwekwa kwenye vyoo vya wanaume hata hivyo kwa bahati mbaya zikapelekwa
mahali kusikohusika.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment