'Beautiful Onyinye' na kipenzi cha Diamond, Wema Sepetu sasa ni
mjamzito. Baada ya misukosuko ya muda mrefu ikiwemo kuporwa na wasichana
wenzake penzi lake la Diamond, sasa Wema amepata kile alichokuwa
akikililia kwa muda mrefu.... Chanzo cha habari hii kutoka kwa marafiki
wa Diamond kimedai kuwa Wema amenasa ujauzito na kugundulika hivyo
walipokuwa Afrika Kusini kwenye tuzo za MTV-MAMA na kumfanya Diamond
achanganyikiwe kwa furaha....
Kwa mujibu wa chanzo hicho, inadaiwa kuwa Diamond kwa sasa kawa kama mtu aliyepagawa kwa furaha kutokana na taarifa hizo njema na tayari ameshaanza maandalizi ya kijacho chake.... Kugundulika kwa
Kwa mujibu wa chanzo hicho, inadaiwa kuwa Diamond kwa sasa kawa kama mtu aliyepagawa kwa furaha kutokana na taarifa hizo njema na tayari ameshaanza maandalizi ya kijacho chake.... Kugundulika kwa
ujauzito wa Wema ni baada ya
kuanza kujisikia vibaya walipokuwa Afrika Kusini ikiwemo kichefuchefu na
kizunguzungu alipokuwa hotelini alipofikia na kulazimika kwenda
hospitali kwa uchunguzi zaidi.... Inasemekana kuwa Wema alisindikizwa na
Aunt Ezekiel kwenda hospitalini waliyekuwa naye huko Afrika Kusini kumpa sapoti Diamond na madaktari ndiyo waliomjuza kuwa anakiumbe tumboni cha wiki 7... Taarifa za madaktari hao zilimfanya Wema awe kama mwehu aliyepagawa na kurudi hotelini kwa mumewe Diamond huku akiwa na tabasamu ambalo hapo awali Diamond hakuwahi kuliona.... Inasemekana kuwa mpaka sasa siyo Diamond wala Wema aliyewaambia wazazi wake kuhusiana na mimba hiyo zaidi ya watu wa karibu wa wawili hao
waliowasindikiza Afrika Kusini.
Source : blogu ya wananchi
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro








Post a Comment
Post a Comment