Dude
“Adam Kuambiana amefariki kweli,chanzo hakijajulikana zaidi lakini kwa taarifa
tulizozipata mwanzo inasemekana asubuhi alijisikia vibaya akaona kama mwili
unaishiwa nguvu hivi,kwahiyo watu wakachukua gari kumpelea hospitali ndo akafia
kwenye gari. Nawapigia sasa hivi simu Mtitu na Stive Nyerere wanaupeleka mwili
hospital, wengi wanasema alianza usiku vidonda vya tumbo.”
Batuli
“Msiba unauma sana, ghafla halafu kijana,inauma sana ninachoweza kuongea kwa
sasa hivi, ni swala moja kwanza kukubali matokeo la pili ni kumuombea,
ameondoka na sisi tunafuata.”
Bondi
“Kweli na mimi nimesikia hivyo, Adam Kuambiana amefariki akiwa location mitaa
ya Sinza, kwahiyo msiba tumeupokea kwa huzuni kubwa ila tumuombee kwa mungu.”
Deogratius Shija
“Nimesikitishwa na kifo cha Adam Kuambiana,lakini pengo la Adam Kuambia ni
kubwa sana, jamaaa alikuwa jembe kwenye filamu, unajua imekuwa ghafla labda ata
angeumwa lakini duh ndiyo hivyo hakuna jinsi tumuachie mungu.”
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment