vifo vyazidi Nigeria
Maafisa nchini Nigeria wamesema kuwa wamepata maiti 118 kufuatia shambulio la bomu katika mji wa Jos.
Mabomu
mawili yalilipuka mojawepo ikiwa imefichwa ndani ya gari na kulipuka
katika soko moja kubwa. Dakika 20 baadaye mlipuko wa pili ulitokea
karibu na hospitali.
Inahofiwa kuwa kuna maiti zaidi zilizonaswa kwenye vifusi vya majengo yaliyo poromoka kutokana na shambulio hilo.
mlipuko wa bomu Nigeria
Kufikia
sasa hakuna kundi lililodai kuhusika na shambulio hilo lakini wengi
wanaamini kuwa Kundi la wapiganaji wa kiislamu la Boko Haram lilihusika.
Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan amejitokeza kukemea mashambulio hayo na kusema kuwa amejitolea kuangamiza kabisa ugaidi.
Mji
wa Jos unatazamiwa kuwa mji mkuu wa jimbo la Plateau ambalo liko katika
eneo la katikati linalo tenganisha kaskazini iliyo na raia wengi zaidi
wa kiislamu, na kusini lililojaa wakristu zaidi.
Chanzo BBC Swahili
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro








Post a Comment
Post a Comment