Kufuatia tabia ya vijana kuuunda makundi ya
uharifu na kuvamia nyumba au watu mchana kweupe na kufanya vitendo vya
uporaji na kupiga huku wakijibatiza majina kama vile mbwa mwitu na panya
road,Kibaka mmoja amejikuta akiuwawa na kundi la wananchi mwenye hasira
kali.
Ishu nzima ilitokea baada ya vijana hao
kuiba pikipiki juzi ya jamaa mmoja na wakati wakiwa wanaondoka ndipo
mmoja wa vibaka hao alipodondoka na wananchi kumshambulia kwa kumpiga na
kufa.
Mazishi ya kibaka huyo yalifanyika leo na
ndipo kundi kubwa la mbwa mwitu wapatao 20 na kuendelea walipovamia
makazi ya watu kwa kuingia kila nyumba kwa kupora mali zao ikiwa ni
pamoja na kuwapiga jambo lililowakasirisha wakazi wa Kigogo Sambusa na
kuamua kuwavalia njuga na ndipo walipomkamata kibaka mmoja na kumuua.
PICHA ZOTE NA Gabriel Ng’osha/GPL<<<<<BOFYA HAPA ULIKE PAGE YETU>>>>>
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment