Umoja wa Mataifa umeliweka kundi la Boko Haram la nchini Nigeria katika
orodha ya makundi ya kigaidi sambamba na kuwawekea vikwazo viongozi wa
kundi hilo.
Hatua hiyo ilichukuliwa hapo jana na imekaribishwa pia na
wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na kutaka kuanza
utekelezwaji wa vikwazo hivyo mara moja. Kwa mujibu wa ripoti hiyo,
vikwazo hivyo vinahusu kuuziwa silaha kundi hilo, kufungwa akaunti za
fedha sambamba na kuzuiwa kufanya safari viongozi wa kundi hilo.
Hatua
hiyo imechukuliwa ikiwa ni baada ya mwezi mmoja tangu kundi hilo
lilipowateka nyara wanafunzi wa kike, suala lililoibua makelele ya ndani
na nje ya nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika. Zaidi ya wanafunzi 200 wa
shule ya sekondari wa Chibok ulioko kwenye jimbo la Borno kaskazini
mashariki mwa nchi hiyo walitekwa nyara tarehe 14 Aprili mwaka huu na
kundi hilo ambapo 53 kati yao walifanikiwa kutoroka.
<<<<Bofya hapa ulike page yetu>>>>
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment