Ni siku nyingine tena tunakutana kwenye lovezone yetu kama ilivyo ada nitakuwa nakuletea maada mbali mbali zinazohusu mahusiano, leo nakuletea maada inayohusu vyakula vinavyoongeza hamu ya tendo la ndoa. tililika na maada hapa chini
PILIPILI
Kama tunavyojua wote mara nyingi chakula ambacho
kimeungwa pilipili hufanya hata mapigo ya moyo kuwa tofauti na wakati
mwingine hata jasho kutoka au kamasi kutoka. Kwenye pilipili kuna kitu
kinaitwa capsaicin ambacho hufanya pilipili iwe na hali ya ukali ambao
huwezesha ubongo kutoa homoni ya endorphins ambayo katika hali ya juu
huleta mgusu wa hisia za raha. Pia pilipili husisimua mfumo wa ufahamu
(nerves) wa ubongo na katika kufanya hivyo huwezesha kumshwa haraka
kimapenzi (kunyegeka) na pia ili ukiguswa au kubusiwa au kunyonywa au
kupapaswa uweze kupata hisia kila sehemu
NAFAKA
Nafaka zina nyuzinyuzi (fibre) na sukari ngumu
(complex sugar) ambazo kusaidia kutunza uzito wa mwili. Nafaka husaidia
katika kuzalisha homoni za testosterone kwenye damu. Na pia nafaka
huwezesha mtu kuwa na nguvu hatimaye kwenda masafa marefu wakati wa
tendo. Kula nafaka nzima kama vile brown bread badala ya white bread,
pia kula nafaka halisi badala ya cornflakes ni jambo zuri
linalokuhakikisha afya njema na mahusiano mazuri ya ndoa yako
MATUNDA NA MBOGA ZA MAJANI.
Mlo wenye matunda na mboga za majani una matokeo
makubwa sana katika hamu ya tendo la ndoa kwa njia nyingi. Kwanza
matunda na mboga za majani hupunguza kiwango cha mafuta na unene
(cholesterol), kuongezeka kwa mafuta mwilini huzuia mzunguko wa damu kwa
kubana mishipa ya damu. Pia kula matunda na mboga za majani huhakikisha
balance ya uzito kwani unene (obesity) kwa wanaume kuna matokeo mabaya
katika kuzalisha homeni za testoeterone na hatimaye jogoo kushindwa
kuwika na kuwa na libido kidogo. Na pia wanandoa wanapozidi kunenepeana
ndipo na hali ya kufurahia au kutaka au hamu ya tendo la ndoa huzidi
kupungua.
TANGAWIZI
Tangawizi ni chakula ambacho husisimua sana mfumo wa
mzunguko wa damu mwilini, na tangawizi zinajulikana sana kwa kusukuma
damu kwenda sehemu za viungo vya uzazi yaani uke na uume. Inaweza kuliwa
mbichi, au kupikwa au kuanikwa na kuwa kama unga.
ASALI
Asali ina madini yanayoitwa boron, ambayo husaidia
mwili kutumia homoni ya estrogen ambayo ni homoni inayohusika na viungo
ya uzazi na mapenzi kwa mwanamke. Pia kuna utafiti unaoonesha kwamba
asali huongeza nguvu, kitendo ambacho kitapelekea mwanamke kuwa uwezo na
hamu ya tendo la ndoa au libido.
KARANGA
Karanga huhusika moja kwa moja na kutunza mfumo wa
mzunguko wa damu kuwa na afya (vascular system). Pia mfumo wenye afya
(mzunguko wa damu) katika uke na uume huwezesha mwanaume na mwanamke
kupata msisimko wa mapenzi haraka hatimaye tendo la ndoa kuwa zuri. Pia
karanga zina madini muhimu kama vile magnesium, asidi ya folic na zinc
ambayo ni muhimu sana katika usalishaji wa mbegu za mwanaume.
OYSTERS
Huwa na kiasi kikubwa sana cha madini ya zinc na
haya madini ndiyo huhusika zaidi na uzalishaji wa homoni ya testosterone
kwa wanaume. Pia imethibitika kwamba wanaume wenye ukosefu wa madini ya
zinc huwa na matatizo ya nguvu za kiume na wakati huohuo kuwa na madini
mengi ya zinc mwilini huongeza kiwango cha shahawa.
SOYA
Pamoja na kuwa na kiwango kidogo sana cha fat na pia
kuwa na kiwango kizuri cha protein, soya zina phytoestrogens ambayo
husaidia sana wanawake ambao wamefikia menopause kutengeneza homoni
estrogen ya ziada. Husaidia uke kuwa laini (wet, lubricated) mwanamke
akisisimliwa wakati wa tendo la ndoa.
CHOCOLATE
Chocolate ina phenylethylamine, kemikali ambayo
husababisha hisia (feelings) za furaha wakati wa mwanamke au mwanaume
kufika kileleni (orgasm)
Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi
Post a Comment
Post a Comment