Milipuko kadhaa imetokea mjini Mombasa nchini
Kenya, ambapo imedaiwa walipuaji wamelipua
sehemu tatu tofauti. Akizungumza kutoa taarifa za
tukio hilo Kamishna wa kaunti ya mombasa Nelson
Marwa, amesema kuwa waliotekeleza shambulizi
hilo huenda wametoroka wakitumia piki piki.
Aidha amesema kuwa watu 3 wamefariki kutokana
shambulizi hilo la guruneti, huku mlipuko
mwingine ukishuhudiwa katika eneo la Nyali Reef,
lakini hakuna majeruhi.
Ikumbukwe kuwa shambulizi hili linajiri siku
chache tu baada ya mlipuko mwingine
kushuhudiwa jijini Nairobi katika kituo cha polisi
cha Pangani ambapo watu 4 wakiwemo maafisa 2
wa polisi walifariki.
Msemaji huyo amesema kuwa maafisa wa polisi
tayari wameanza kuwasaka washukiwa wa matukio
hayo.
Repoti kutoka Shirika la Msalaba mwekundu,
inasema kuwa waliofariki ni watu watstu akiwamo
mwanamke mmoja na wanaume wawili.
Walijeruhiwa 25,kwa sasa waliojeruhiwa
wanaendelea na matibabu ikiwa ni pamoja na xray
na ukaguzi mwengne.viongozi wa kaunti wa msa
wamefika.
TUNAOMBA RADHI KWA PICHA HIZI..!! ,MLIPUKO ULIOTOKEA MOMBASA WAUA WATU 3
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment