
Tume ya uchaguzi ya Malawi imesema itatangaza matokeo ya uchaguzi ijumaa.
Hatimaye tume ya uchaguzi nchini Malawi imesema itatangaza matokeo ya uchaguzi mkuu wa nchi hiyo kesho ijumaa.
Uamuzi huo unakuja baada ya mivutano na mapingamizi kadhaa kwenye mahakama kuu nchini humo.
Mwandishi wa BBC Baruan Muhuza ameeleza kutoka
mji mkuu wa nchi hiyo Lilongwe kuwa sasa wananchi wa Malawi wameondolewa
hofu ya kusubiri kwa muda mrefu matokeo ya kura za uchaguzi walioufanya
juma lililopita.
Taarifa fupi iliyotolewa na tume ya uchaguzi
jana usiku mjini Blantyre, imesema wameamua kutangaza matokeo hayo kwa
kuzingatia sheria inayoibana kufanya hivyo ndani ya siku zisizozidi nane
na ikiwa ni baada ya saa 48 tangu kumaliza hesabu ya kura.
Kwa siku mbili sasa kumekuwa na tuhuma za
kuokotwa kwa baadhi ya masanduku ya kura, huku baadhi ya magari ya
yakipatikana na masanduku ya kura na hata katika baadhi ya maeneo ambako
ilielezwa kuwa kura zimehifadhiwa, usalama wake umesemwa kuwa mdogo.

Tume ya uchaguzi ya Malawi imesema itatangaza matokeo ya uchaguzi ijumaa.
Tangu jumatatu tume hiyo imekuwa ikisubiri
uamuzi wa mahakama kuu mjini Blantyre wa kuiongeza muda wa angalau siku
30 kukamilisha jukumu ililopewa, hata hivyo mahakama yenyewe bado ina
mashauri mengine iliyopokea kuhusu uchaguzi huu
Mmoja kati ya wananchi wa nchi hiyo
aliyejitambulisha kwa jina la Malani Nyirenda, alielezea hisia zake
alipozungumza na BBC mjini Lilongwe kutokana na suala la kuchelewa
kutolewa matokeo na mpango wa kuhesabu upya kura za baadhi ya maeneo.
Tume hiyo imesema hadi kufikia sasa imepokea malalamiko 275 na imekwisha yafanyia kazi malalamiko 170 tu.
Chanzo bbc
BOFYA HAPA LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment