Serikali
ya Malaysia, imetoa data iliyotumika kuthibitisha kuwa ndege ya Malaysia
iliyotoweka MH370 ilianguka kusini mwa bara Hindi.
Data hiyo
ilitolewa kwanza kwa jamaa wa abiria wa ndege hiyo ambao wamekuwa
wakitaka maafisa wakuu kutoficha taarifa zozote kabla ya vyombo vya
habari kutoa taarifa hiyo.
Data hiyo iliyotolewa Jumanne,ni ya kurasa 47 pamoja na maelezo mengine kutoka kwa kampuni ya uingereza ya Inmarsat.
Ndege ya MH370 ilitoweka tarehe 8 mwezi Machi, ilipokuwa safarini kutoka Kuala Lumpur kuelekea Beijing.
Ilikuwa imewabeba watu 239 wengi wakiwa raia wa Uchina.
Tangu kupotea , ndege hiyo haijaonekana na hakuna sababu iliyotolewa ya kupotea kwa ndege yenyewe.
Data
iliyotolewa inaonyesha mawasiliano ya kawaida kati ya marubani na na
mtambo wa Satelite ambayo yaliwasababisha wachunguzi kufikia kuwa ndege
hiyo ilimaliza safari yake nchini Australia.
Wakati
huohuo, msako wa chini ya bahari kuitafuta ndege hiyo kwa kutumia
Manowari ya Roboti, bado unaendelea mjini Perth, Australia.
Manowari hiyo imekabidhiwa kwa Australia kwa mkopo.
Kadhalika
manowari yenyewe kwa jina Bluefin-21, ambayo ina uwezo wa kuona vifaa
vidogo sana chini ya bahari, ilianza tena kazi yake wiki hii baada ya
kupatwa na hitilafu na kurekebishwa.
Inatarajiwa kuondoka katika eneo hilo Jumatano na kurejea kwa kazi tena tarehe 31 mwezi Mei.
Manowari
hiyo ilimaliza shughuli za mwanzo kutafuta ndege hiyo baada ya taarifa
za kuwepo vinasa sauti vya ndege hiyo iliyotoweka baharini ingawa
havikupatikana.
Serikali
ya Australia sasa inajiandaa kwa msako mwingine chini ya bahari kwa
kutumia vifaa maalum vilivyokodiwa.
Chanzo BBC Swahili
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment