Mwanamuziki Rehema Chalamila ‘Ray C’,
ametoka katika Hospitali ya Mwananyamala,
Dar es Salaam alikokuwa amelazwa.
Mwanamuziki huyo ambaye amekuwa katika
tiba ya kuachana na matumizi ya dawa za
kulevya hospitalini hapo, alifikishwa hapo juzi
Jumatatu asubuhi na baadhi ya madaktari
walibainisha kuwa Ray C alikuwa
anasumbuliwa na ugonjwa wa dengue ambao
umelipuka katika maeneo mengi jijini Dar es
Salaam hivi karibuni.
Akizungumza kwa simu jana, Ray C alisema
ameondoka hospitalini na yuko nyumbani
baada ya kuruhusiwa na madaktari.
Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Dk Sophinias
Ngonyani alisema mwanamuziki huyo
aliruhusiwa baada ya kupata nafuu na hali
yake kuonekana nzuri. <<<<<<BOFYA HAPA ULIKE PAGE YETU PLEASE>>>>
Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi
Post a Comment
Post a Comment