WASANII nyota wa vichekesho Bongo,
Ulimboka Mwalulesa ‘Senga Kijumule’ na swahiba wake, Yusuph Kaimu
Machoti ‘Pembe’ hivi karibuni walifunga mtaa mjini Kahama baada ya
mashabiki kuwazunguka kwa dakika 45 wakiwashangaa.
Wasanii nyota wa vichekesho Bongo, Ulimboka Mwalulesa ‘Senga Kijumule’(kulia) na swahiba wake, Yusuph Kaimu Machoti ‘Pembe’.
Wawili hao ambao walijipatia umaarufu
mkubwa wakati walipokuwa wakiigiza kupitia televisheni, walikuwa katika
Wilaya za Mbogwe na Kahama wakati wa uzinduzi wa albamu ya tatu ya
msanii wa muziki wa asili wa Kabila la Wasukuma aitwaye Bhudagala.
Baada ya wananchi kuwaona wasanii hao
wakitembea kwa miguu katika mitaa mjini hapa, walianza kuwafuata
taratibu na hatimaye kujikuta wakiwa kundi kubwa ambalo halikutarajiwa.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro








Post a Comment
Post a Comment